"Vyombo vya ulinzi na usalama mahala pao ni barracks, ni vituo vya polisi, ni kwenye kazi za kiintelijensia, sio siasa. Siasa iachwe ifanywe na wanasiasa. Vyombo viwe delinked na siasa, na wao wajibu wao ni kutumikia yule ambaye umma umemtaka. Tukishafanya hiyo hatua, tutakuwa tumepiga hatua kuwa na inapaswa iwe kampeni, kwa sababu ni vigumu, wana enjoy, kwa sababu kuwatoa kwenye comfort zone haitakuwa kazi rahisi, lakini lazima iwe ni vita ambayo kila mtu aipigane, kila mtu.
Na mimi kwa kweli kila nikipata nafasi hili nalizungumza kwa uwazi kabisa kwamba, kinachoitwa the elephant in the room katika demokrasia yetu, katika namna ya kusogea mbele nchi yetu, ni vyombo vya ulinzi na usalama.
The day tunafanikiwa kuviondoa vyombo vya ulinzi na usalama kwenye siasa vikafanya kazi zao kwa weledi, hatua tutakayokuwa tumepiga ni hatua kubwa sana. Na haina maana kwamba hatujawahi kufika huko, tumewahi.
Mkapa alipeleka sheria bungeni mwaka 1996 ya National Intelligence and Security Act, ambayo Section 5 ya ile sheria sio tu imezuia vyombo hivyo, mfano Idara ya Usalama, kushiriki kwenye siasa moja kwa moja, ilizuia hata kukamata. Yaani kwamba, intelligence officer hana wajibu wa kukamata, wajibu wa kukamata ni wa polisi.
Mwaka 2023 tumeenda kufanya amendment ya hiyo sheria bungeni, sio tu tumewapa mamlaka ya kukamata, tumewapa hata mamlaka ya kubeba silaha. Hawakuwa na hiyo mamlaka, na ndio maana utekaji umeongezeka. Na ndio maana mnasikia watu wasiojulikana. Watu wasiojulikana ni nani wenye pingu?
Tumebadilisha sheria sisi wenyewe, yaani tumerudi nyuma badala ya kupiga hatua ya mbele. Kwa hiyo lazima na hili mimi nawasihi hata wanasiasa wengine wa vyama vyote, kwa sababu hili haliathiri vyama vya upinzani peke yake, linaathiri pia hata watu ndani ya CCM, kabisa.
Na mkishakaa nao private wanakuambia, eh kwamba Idara kuingilia shughuli za ndani ya CCM ina maana kwamba Idara inachomeka watu wake inayowataka na haitoi ule uhuru wa wao kama CCM kufanya na nani zao. Sasa, watu wanaweza wakaona ah, haya ni mambo ya CCM, hapana. Watafanya hivyo CCM, watafanya hivyo vyama vya upinzani pia, watasubiri kwenye uchaguzi mkuu. Kwa hiyo ni lazima iwe ni vita ambayo kila mtu ambaye anataka nchi yetu irudi kwenye reli, kila mtu aseme imetosha, turudi."