Pre GE2025 Zitto: Uchaguzi wa 2024 unaweza kusimamiwa na Chombo ambacho hakipo Kisheria

Pre GE2025 Zitto: Uchaguzi wa 2024 unaweza kusimamiwa na Chombo ambacho hakipo Kisheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Zitto.png

Mwanasiasa wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Sheria mpya ya Tume ya Uchaguzi imefuta Sheria zote za uchaguzi wa zamani na hivyo TAMISEMI imefutwa rasmi kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Amesema “Sheria ya Uchaguzi bado haijatungwa, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa uchaguzi wa 2024 kusimamiwa na Chombo ambacho hakipo katika Sheria. Hilo ni jambo ambalo Waandishi wanatakiwa kuwa nalo makini na kulifuatilia kujua kwa nini Sheria haijatungwa mpaka sasa.

Ameongeza kuwa changamoto katika chaguzi ikiwemo suala la uwepo wa Kura Bandia bado lipo akidai hivi karibuni Mkoani Kigoma, vijana wa ACT Wazalendo walikamatwa na kufikishwa Mahakamani licha ya kuwa wao ndio walioripoti uwepo wa Kura Bandia
 
Back
Top Bottom