Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Tumeona uzinduzi wa kampeni za vyama pendwa vya siasa! Chadema wameanza ,wakaja cuf na kumalizia na act wazalendo!! Nilichojifunza ni kwamba act wazalendo wanakaa chini na kuandaa hotuba zao !! Utaona kuanzia msemaji wa kwanza mpaka wa mwisho hoja zao zimepangiliwa na zinaeleweka sana ! Zinagusa wananchi na zinatoa malalamiko na ufumbuzi wa Nini kifanyike!! Chadema wanaonekana hawana muda wa kukaa na kupangilia hotuba Kila mtu ana panda jukwaani na hotuba yake kichwani !! Hawana lengo wanalopigania HASWAA!! Wengi wakisimama wanaongelea matukio na uongozi wa magufuli kana kwamba anawasikia au Bado Yuko hai !! Zitto kabwe ni mwanasiasa aliyeiva HASWAA !! Hana haraka na mambo na hakurupuki bila tafakuri na huwezi kumkuta amelewa akiwa anahutubia!! Viva zitto kabwe !! Viva act wazalendo!