Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

Zitto kwanini unashindwa kutamka hadharani kwamba wewe na ACT Wazalendo mnaunga mkono Lissu awe mgombea urais wa upinzani?
Kauli zako zimekaa kimitego mitego sana badala ya kuwa mstari wa mbele kuonyesha ushirikiano wa kweli.
 
Baada ya kumuona BM hauziki Zitto anawaza ruzuku
Nasubiri hiyo October, nione ninyi wabinafsi mtakavyoshindwa uchaguzi. Yaani Lissu anataka ushirikiano kutoka moyoni na anajua ndiyo njia pekee ya kupata ushindi lakini wapambe wa Chadema ni wabinafsi kupita maelezo??!!
 
Pendekezo la watanzania wengi ni kuona Membe akimpa support Lissu!! pia CDM nao kwa umoja wao wakimpa Support Maalim kule Zanzibar.
Acheni upuuzi. Eti CDM atampa support Maalim Zanzibar kwa ushawishi upi walionao CDM Zanzibar. Chama hakina hata mbunge mmoja wala shekha. Yaani Chadema kuanzia viongozi hadi wanachama ni matapeli.
 
..Lowassa alipokelewa ikulu.

..Babu Seya na Papii walipokelewa ikulu.

..Je, hujamuona Papii anatumbuiza ktk matamasha ya ccm?

..sera ya kulawiti watoto ni sera ya ccm.
Sera ya watu wazima kulawitiana ni ya mgombea wa sasa wa Chadema,

Alisema wazi kabisa kuwa ataruhusu ushoga.
 
Mbowe is very selfish.

But, too bad he's on a losing side.

Zitto hata akipata wabunge 5 ni hatua kubwa sana.

Losing side kwa Chama chenye mbunge mmoja na madiwani 10 na usheeeeeeeee nchi nzima?hahahahah
 

Jambo usilolijua ni kwamba ACT ni ya Kikwete ndo maana Membe kaenda huko kwenye chama cha kaka yake na strategically chama hiki kiliundwa kudhoofisha CDM na Zito analifaham vizuri hili na yeye ndiye alikabidhiwa kazi hiyo maalum.

Watz wanataka mabadiriko na Lissu atosha ni Bora tubaki wenyewe na Lissu wetu na si kuchangamana na Chui walovaa ngozi ya Kondoo na Zitto si wa kuamini hata kidogo kwani yeye ni mtu wa kucheza na fursa na mnafiki in English he is Opportunistic and Hypocrite.

Siwezi msahau alivyoiuza chadema kipindi kilena kuwatengeneza akina Juliana Shonza na Martin Shigela ambao sasa hivi wanavyeo ndani ya ccm.
Nadhani ni muda muafaka chadema kutambua hilo na tusimame wenyewe na Tundu Antiphas Mughwai Lissu. Hawe wengine bado wapo sokoni
 
Vijiji havitampigia kura. Asalimu amri tu kwa Dokta Magufuli kamanda wa kudhoofisha upinzani nchini
Ni mtizamo wako mkuu siwezi kukupinga maana mpaka mwanakijiji anakubali kwenda kwa lissu hauwezi jua atafanya kitu gani kwenye sanduku kwasababu hajapuuza uwepo wake na ndio maana kuna wengine hawakwenda./hakusepa nao.
 
Ni mtizamo wako mkuu siwezi kukupinga maana mpaka mwanakijiji anakubali kwenda kwa lissu hauwezi jua atafanya kitu gani kwenye sanduku kwasababu hajapuuza uwepo wake na ndio maana kuna wengine hawakwenda./hakusepa nao.
Walienda kumshanga mtanziaaa pekee mwenye ujasiri wa kumkosoa Magufuli hadharani.
 
Nakubaliana naye kabisa vyama vya upinzani vitoe mgombea mmoja kwenye kila nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani baada ya wagombea wa vyama vyote kujulikana.

Wasiangalie ni Chama gani kina wafuasi wengi bali waangalie ni mgombea gani wa upinzani anakubalika zaidi na wapiga kura wa eneo husika.

Bila kujali vyama, mgombea huyo akipatikana, wagombea wengine wote wa vyama vya upinzani na wafuasi wao wote wamuunge mkono huyo mmoja wa upinzani dhidi ya yule wa Chama tawala.

Ushindi utakaopatikana utakuwa ni wa vyama vyote vya upinzani na kuunda Serikali yao kwa taratibu walizojiwekea na kukubaliana. Wananchi wanasubiri kwa hamu hiyo Serikali .
 
Kwenye majimbo kila mtu ale kwa usawa wa kamba yake kwenye Urais wekeni mtu mmoja
2015 watu hawajasahau, na pia wenzako bungeni walivyopinga uchafuzi wa kina Jecha Zanzibar baada ya Shein kuingia bungeni wewe Zitto ukawa upande ule, hivyo usilazimishe mambo kwa kuweka wingi wetu eti 'Watanzania hawata tusamehe"
Aache janja ya nyani hapa
 
Hadi muda huu kama wapinzani hawajapata mtu wa kusimama basi wamekwisha.
 
Tangu lini jamaa analipenda Taifa hili.

Alisema tuna Korona.

Akawa anapiga kampeni tunyimwe fedha za World Bank.

Huu upendo wa dhati kwetu umekuja kipindi anataka kura sio??
Naongezea tu, kwa nin zzt ameleta mgombea si angesema sisi tunasimama na chama flani kama ilivyofanya TLP ya Mrema
 
Amesahau 2015
 
Zitto kama alikuwa na nia ya dhati basi angemshauri Membe aende CHADEMA!
Asingekuwa na bargaining chip...Kwa SASA ata akipiga simu inapokelewa...lakini pia Kwa target yake ni kupata wabunge kutoka maeneo alipotokea recruit wake mpYA
 
Zzt alidhani atatumiwa kama 2015
 
Lissu kwa maneno yake na vitendo vyake anashindana Magu na CCM kwa ujumla kwenye huu uchaguzi. Chadema wengine waliobaki wanapambana na ACT kuwa nani ni mpinzani zaidi ya mwenzake na ataunda kambi ya upinzani hiyo 2020. Patamu hapo. Yetu macho.
 
Ye ameshasamehewa? Maana 2015 alishiriki kwenye kuharibu kura za UKAWA.ZZK kuna wakati huwa namuona kama sio mpinzani hata Maalim Seif awe makini na ZZK
Maalimu pale kaingizwa mkenge, zito ni lipumba type, anafikiri watu ni wasahaulifu, aliwaita wenzake wa ukawa kuwa ni wasaka tonge, ni ngumu kufanya kazi na mtu ambaye ameonyesha dhahili sio wa kuaminika, na hili ndilo linawafanya cdm kuwa wazito, kwanza kitendo cha kumpokea membe na kumfanya kuwa mgombea wao, ni ishara tosha hakuna kitu cha kusimisha mgombea moja, sasa wanajidanganya kwa membe eti ni turufu ya kusini, sasa huyo membe mwenyewe hata kuongea hawezi, ni bora angebaki na u tiss wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…