Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

MOSintel Inc

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2016
Posts
817
Reaction score
593
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ametoa wito kwa vyama vya upinzani nchini kuwa viache ubinafsi kwa kuwa Tanzania ni kubwa kuliko vyama na kwamba Watanzania hawatowasamehe kama hawatoamua kuwa na mgombea mmoja wa Urais, Ubunge na Udiwani.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 18, 2020, Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa mpaka sasa viongozi wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya vyama hivyo kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao na anaamini kuwa Watanzania wengi wanataka mashirikiano.

Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo,na kila Kata, wito wangu kwa viongozi wenzangu wa vyama vya upinzani tuache ubinafsi, Watanzania wanataka ushirikiano ili kuleta mabadiliko katika nchi, na joto la uchaguzi mmeliona watu wamechangamka Bara na Visiwani" amesema Zitto Kabwe.

Zitto ameongeza kuwa yeye na chama chake wako tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuweza kuitoa CCM madarakani.

Chanzo: EATV

Nini maoni yako?
 
Mgombea mmoja ni lazima awe Tundu, achaneni wa wale watakaorudi kundini(nyumbani kwanoga)! Kama siyo hivyo basi yaendelee kama ilivyokuwa 2015!!!! kwani wapinzani walijikoroga wenyewe kwa kumuita Lowassa wa upinzani “fisadi” na sasa karudi kundini. Mzee wa Mtama hivyo hivyo atarudi kundini
emoji23.png
emoji23.png
 
Kuhusu Membe kumpa support Lissu nakubali.

Kuhusu eti CHADEMA kusema mtasupport Maalim Seif Zanzibar huo ni UTAPELI wa Kimangi.

🖕🖕

Tz tunatakiwa tubakie na vyama vifuatavyo; NCCR, ACT, CCM, na CDM.

Na itapendeza vyama hivyo vikiwa na nguvu zinazokaribiana.

Tukibakiwa na vyama viwili, siasa zetu zitakuwa kama za Zanzibar ambapo kuna mkwamo.

Nchi hii ni kubwa na ina watu wengi, hivyo inaweza ku-accomodate vyama zaidi ya viwili au vitatu vya siasa.
 
Back
Top Bottom