Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

Mgombea urais awe TL
Zanzibar hiyo ni Maalim Seif
Kwenye bunge na udiwani huko kila chama kiende kivyake. ZZK yupo kwa ajili ya kukuza chama chake. Pia wengi tunahisi kwamba akipewa pesa ya kutosha aweza uza mechi na timu pia
 
Zitto kwanini unashindwa kutamka hadharani kwamba wewe na ACT Wazalendo mnaunga mkono Lissu awe mgombea urais wa upinzani?
Kauli zako zimekaa kimitego mitego sana badala ya kuwa mstari wa mbele kuonyesha ushirikiano wa kweli.
Mkuu kwanini aseme yeye wakati nae ana chama chake na lazima angalie maslahi ya chama chake sio kuunga mkono tu, hapa kila mtu anapambania maslahi yake ila atakae poteza zaidi ni kwa mtazamo wangu ni CHADEMA na Watanzania, Wakisimama wagimbea watatu Lissu, Magufuli na Membe wala CCM hawana haja ya figusu watashinda maana wapinzani watagawana kura vivyo hivyo kwenye majimbo na udiwani mwisho wa siku ACT ina strong base yake visiwani haiyumbi hiyo na siasa za kule zinatambulika ila huku bara upinzani utapotza vibaya, Uchaguzi ni zaidi ya kujaza watu nnachoona kuna watu wanajiona wana hati miliki ya upinzani na hawaanglii maslahi ya taifa bali ya vyma vyao na kwahivyo hakuna namna CCM inaweza kutikiswa.
 
Umewasikia viongozi wa Chadema wakiropoka ropoka hadharani kuhusu hii issue zaidi ya kusema wanataka na wanakaribisha ushirikiano na chama cha Zitto?

Kwanini zitto anaendelea kuropoka ropoka hadharani badala ya kujadiliana nyuma ya pazia?

Membe ana mwezi tu upinzani kwanini yeye apewe kipaumbele ukilinganisha na aliye upinzani zaidi ya miaka 20!?
😳😳😳

Mkuu kwanini aseme yeye wakati nae ana chama chake na lazima angalie maslahi ya chama chake sio kuunga mkono tu, hapa kila mtu anapambania maslahi yake ila atakae poteza zaidi ni kwa mtazamo wangu ni CHADEMA na Watanzania, Wakisimama wagimbea watatu Lissu, Magufuli na Membe wala CCM hawana haja ya figusu watashinda maana wapinzani watagawana kura vivyo hivyo kwenye majimbo na udiwani mwisho wa siku ACT ina strong base yake visiwani haiyumbi hiyo na siasa za kule zinatambulika ila huku bara upinzani utapotza vibaya, Uchaguzi ni zaidi ya kujaza watu nnachoona kuna watu wanajiona wana hati miliki ya upinzani na hawaanglii maslahi ya taifa bali ya vyma vyao na kwahivyo hakuna namna CCM inaweza kutikiswa
 
You know what they say ‘desperate times, calls for desperate measures’.

Ina maana ACT awajiamini wenyewe.
 
Huyu ndiye mzalendo wa kweli maana ana hofu ya mungu na anafuata taratibu na kanuni za uchaguzi unapotafuta wadhamini. Siyo yule mpayukaji anaofanya watu waache shughuli zao waende kumshangaa

Hakuna mtu yoyote kalazimishwa kwenda kumuona Lisu.
 
Zito aachane na mambo ya kuungana maana hayana mwisho mwema, maana kila chama kina falsafa zake. Ni vyema wawe na agenda za pamoja wakipanda jukwaani. Haya mambo ya muungano isiyo na utaratibu maalum, huwa inatumika kudhoofisha vyama na kuishia kuchafuana tu.
 
Zitto ameanza kazi rasmi. Wapinzani mpaka wavurugane aisee
 
Mkuu, sera za ccm nikuendeleza yale mambo yote yalianzishwa na watangulizi sasa yeye ameunganisha wote kuanzi awamu ya kwanza hadi ya nne. Hapa ni kazi tuu, na kazi inaendelea

Watu wanaochagua kwa kuangalia sera nchi hii ni wachache sana, watu wengi huchagua kwa hamasa, mahaba niue, mazoea, kupewa rushwa nk. Ccm hawategemei sera kushinda usitake kupotosha, vinginevyo tusingeona uchaguzi wa SM za mitaa ukinajisiwa. Kama wakoloni walijenga miundombinu wakati walikuja kuchuma, unategemea chama gani kitashindwa kufanya chochote kama kinakusanya kodi? Hilo neno sera linatamkwa kama fashion tu, lakini 70%+ ya wapiga kura hawachagui kwa kujali sera.
 
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ametoa wito kwa vyama vya upinzani nchini kuwa viache ubinafsi kwa kuwa Tanzania ni kubwa kuliko vyama na kwamba Watanzania hawatowasamehe kama hawatoamua kuwa na mgombea mmoja wa Urais, Ubunge na Udiwani.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 18, 2020, Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa mpaka sasa viongozi wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya vyama hivyo kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao na anaamini kuwa Watanzania wengi wanataka mashirikiano.

Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo,na kila Kata, wito wangu kwa viongozi wenzangu wa vyama vya upinzani tuache ubinafsi, Watanzania wanataka ushirikiano ili kuleta mabadiliko katika nchi, na joto la uchaguzi mmeliona watu wamechangamka Bara na Visiwani" amesema Zitto Kabwe.

Zitto ameongeza kuwa yeye na chama chake wako tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuweza kuitoa CCM madarakani.

Chanzo: EATV

Nini maoni yako?
Well said
 
Sasa mbona kaishachelewa? wenzake wanachanja mbuga yeye ndiyo anaamka kashikilia mswaki? pole zake. Membe yuko Mkoa gani kwa sasa?
Wadhamini hawahjtaji mapokezi mkuu. Huoni JPM anawakusanya kimya kimya.
 
Huyu ndiye mzalendo wa kweli maana ana hofu ya mungu na anafuata taratibu na kanuni za uchaguzi unapotafuta wadhamini. Siyo yule mpayukaji anaofanya watu waache shughuli zao waende kumshangaa
Mkuu mbona upo too harsh!
 
Back
Top Bottom