Zlatan Ibrahimovic atua rasmi Manchester

Zlatan Ibrahimovic atua rasmi Manchester

Majighu2015

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
2,937
Reaction score
3,959
Manchester, Uingereza.

Mchezaji wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amejiunga rasmi na klabu ya Manchester United ya Uingereza huku akitamba kuandika kumbukumbu mpya katika historia ya ligi ya England.

Mchezaji huyo aliyekuwa akicheza na klabu ya PSG ya Ufaransa amesaini mkataba wa mwaka mmoja na tayari kocha wake Jose Mourinho amesema kuwa haihitaji kutoa sababu nyingi kuelezea kwa nini ameamua kumsajili mshambuliaji huyo kwa vile ‘ takwimu zinajieleza’.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza wakati walipokuwa katika klabu ya Inter Milan ya Italia na kwamba sasa wanakutana tena wakiwa nchini Uingereza.

Ibrahimovic ambaye amekuwa akisifika kwa kupachika mabao ya kushtukiza ameandika kwenye mtandao wake wa Twitter akisema kuwa ‘”ninayo furaha kubwa kujiunga na klabu hii lakini jambo kubwa kwangu ni kufanya kazi tena kocha Jose”

Hongereni man utd. Kifaa hicho ingawa ni kibabu.
 
mwaka 2010 wakati samwel eto'o anahama kutoka barca kwenda inter wakipshana na ibra cadabra aliekuwa anatoka inter kwenda barca, jose mourinho aliyekuwa kocha wa inter,alinukuliwa akisema barca wamebadilisha rungu kwa bunduki, leo ndo nimeelewa alikuwa na maana gan
 
Moja ya jambo lakujivunia sana katika usajili wa 2016 ni kumchukua Ibra Kadabra. a.ka "the Master"

Sababu moja kubwa ni ile wazungu wanasema transformation of experience during construction phrase" hii naiona inalenga sana uwepo wa vijana mashuhuri (superyouth) Rashford, Martial, Lingard na wengine. chini ya usimamizi (mentaling) ya Ibrahimovic naiona safu bora kabisa kuwahi kutokea pale OT.

Kimsingi pamoja na kuletwa kusaidia lakini kikubwa ninachokiona ni transformation ya experience aliyonayo kwa vijana ujuzi wa level za juu kabisa. Ikumbukwe Wyne Rooney hana character za ibra hivyo ibra anaweza kuwa roll model mzuri sana kwa vijana waliopo pale OT kwa sasa
 
Back
Top Bottom