The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Zoezi la uchukuaji wa fomu nafasi za Ubunge na Udiwani, limeanza leo rasmi kwa baadhi ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi mkuu mwaka huu, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya, huku uteuzi wa wagombea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chaumma ukisubiriwa kwa hamu kujua watakaoteuliwa rasmi kugombea nafasi hiyo.
Bw. Sarif Venance, Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Mbarali, amesema baadhi ya wagombea wa vyama mbalimbali vya uchaguzi leo wameanza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo ofisi ndogo ya tume huru ya taifa ya ya uchaguzi (INEC) Wilaya ya Mbarali kwa ajili ya kuanza safari ya kupata kiti cha Ubunge na Udiwani.