Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Nakumbuka siku chache baada ya Bunge kuvunjwa,nilitoa pendekezo kupitia Jukwaa hili la Siasa nikipendekeza wabunge wa CHADEMA waliomudu kumaliza ubunge wao wakiwa ni wabunge wa chama hicho wapewe vyeti kama njia mojawapo ya kuwapongeza kumaliza ubunge katika mazingira magumu waliokuwa nayo, na pia kwa kusimama imara na kukataa kurubuniwa kwa vyeo au vipande thelathini vya fedha ili wasaliti wapiga kura wao.
Bila kujali kama walisoma wazo langu na kuamua kulifanyia kazi au na wao teyari walikuwa na wazo kama hilo,nafurahi kuona jambo hili linafanyika na linaendelea kufanyika kwa wabunge hawa kupewa vyeti na ofisi zilizoko katika majimbo yao.
Hata hivyo,nadhani ingekuwa bora na ingependeza zaidi kama jambo hili lingefanywa na CHADEMA Taifa ambapo Katibu Mkuu angeandaa vyeti hivi na wabunge wangekabidhiwa vyeti hivyo na Mwenyekiti Taifa au mtu mwingine yoyote ambae angeteuliwa kuwa mgeni rasimi, na ninahakika zoezi hili lingepata uzito mkubwa zaidi na pia lingepata coverage kubwa zaidi ya media kuliko ilivyo hivi sasa.
All in all,hongereni sana kwa kuona umuhimu wa jambo hili, ila msisahau kufanya hivi na kwa madiwani wote nchi nzima ili wasijihishe kutengwa(wakawa demoralized) kwani na wao kuna wenzao wengi tu walisaliti chama na pia kuwapa na wao vyeti kutaondoa uwezekano wa jambo hili kufanyiwa propaganda kuwa mmewapuuza madiwani waliosimama imara kwa miaka yote mitano(mmewabagua).
Ni ushauri tu kwa nia njema ya kujenga CHADEMA Imara.