Zoezi la kuondoa Machinga limefanikiwa?

Zoezi la kuondoa Machinga limefanikiwa?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
1. Tathmini ya kuondoa Machinga ikoje?
2. Zoezi limefanikiwa?
3. Kama halijafanikiwa kikwazo ni nini?
4. Kama limefanikiwa nini cha kujifunza kwa baadaye?
5. Miji imekuwa misafi sasa?
6. Foleni zimepungua?
7. Wenye maduka wako huru?
8. Mitaa ya katikati ya miji inapitika?
9. Mitaro inaweza kupitisha maji ya mvua?
10. Makusanyo ya TRA yamepanda?
 
Kwa maoni yangu.....
-Kiujumla ni zoezi la kubahatisha, kujaribu na kupita.
-Kuna mahali limefanikiwa, kuna mahali halijafanikiwa, lakini yote kwa yote ni zoezi linalohitaji kupimwa baada ya miezi sita kuona limezaa nini.
 
15 November 2021

Jiji Letu Baada ya Machinga kupangwa



Source : Malango travels
 
1. Tathmini ya kuondoa Machinga ikoje?
2. Zoezi limefanikiwa?
3. Kama halijafanikiwa kikwazo ni nini?
4. Kama limefanikiwa nini cha kujifunza kwa baadaye?
5. Miji imekuwa misafi sasa?
6. Foleni zimepungua?
7. Wenye maduka wako huru?
8. Mitaa ya katikati ya miji inapitika?
9. Mitaro inaweza kupitisha maji ya mvua?
10. Makusanyo ya TRA yamepanda?
Ngoja kwanza tumalizie usafi kwa kuchoma moto
 
Dar es Salaam
16 November 2021

Jiji Letu Dar es Salaam


 
Dar es Salaam
Jiji la Dar es Salaam lapumua

Machinga baada ya kupangwa, watambuliwa rasmi sasa mikopo, vifaakazi kuwafuata maeneo yao waliopangwa kwakuwa wanatambulika

 
Miezi sita iliyopita kabla ya machinga kupangwa miji ilikuwa imezongwa kupita kiasi kwa kukosa mpangilio

11 May 2021
Mwanza Tanzania


Kabla hali ilikuwa mbaya kwa wote yaani wakaazi wa mji, malori na machinga wenyewe



Usalama na maisha ya wafanyabishara ndogondogo (Machinga), wateja wao na watumiaji wengine wa barabara yako hatarini kutokana na wafanyabiashara hao kupanga bidhaa kwenye njia za waenda kwa miguu hadi barabarani. Kutokana na hali hiyo waenda kwa maiguu wanalazimika kupishana na magari pale wanapopita katika maeneo mbalimbali walipo wafanyabiashara hao huku wengine wakilazimika kusogeza bidhaa zao ili kupisha magari yapite kisha kuzirejesha. Miongoni mwa maeneo ambayo wafanyabishara hao wamepanga bidhaa zao ni katika mzunguko wa Nyerere unaounganisha barabara ya Pamba, Nyerere, Kenyatta na Uhuru jijini Mwanza.
 
Kumenoga Jijini Mwanza baada ya machinga kupangwa, Zoezi lafanikiwa .

Kujipanga ktk kutekeleza agizo la kuwahamisha machinga waliosambaa katikati ya miji kuhamia katika maeneo rasmi waliyotengewa kwa ajili ya kufanya shughuli zao, YuboxTv imekuletea muonekano halisi wa baadhi ya mitaa katika jiji la Mwanza, Tanzania inavyoonekana baada ya machinga kuondoka.
 
Back
Top Bottom