Wadau, kama mjuavyo ni kuwa, kuanzia chana jioni, bunge maalum limeanza zoezi la kupitisha kanuni za bunge hilo. Hii ni baada ya Rasimu ya Pili ya Kanuni hizo kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Kanuni, Prof MAHALU. Busara zilizotumika za wazee kuzungumza kutuliza jaziba miongoni mwa wabunge zimesaidia sana mchakato kuufanya uwe wa kistaarabu tofauti na ilivyokuwa inatafsiriwa hapo awali.
Kwa siku ya jana kuanzia saa 1 usiku hadi saa 3 usiku, jumla ya vifungu 3 kati ya 87 vya Rasimu ya Kanuni hiyo zimepitishwa baada ya kufanyika marekebisho. Kwa siku ya leo kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 8 mchana, Bunge hilo maalum limepitisha kuanzia vifungu vya 4 hadi 10 na zoezi litaendelea kuanzia saa 11 jioni. Hata vile vifungu vilivyoonekana kuwa vinaweza kuwa na msuguano, msuguano huo haukuhatarisha mjadala wa bunge na wote walishirikiana kutafuta ufumbuzi wa pamoja.
Nawapongeza sana wabunge wa bnge letu na hakika wanatuwakilisha vema wananchi. Ni vema wakaendelea kufanya kazi kwa maslahi ya taifa bila ya kushurutishwa na baadhi ya watu ambao imeelezwa kuwa wana malengo yEEa kuvuruga mchakato huu