Zoezi la sensa lisitishwe kwa mwaka 2022, hadi uchumi utakapokaa sawa

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Ni karibia mwezi sasa tangu Urusi apewe vikwazo ambavyo vilitarajiwa kumuumiza ila kwa kuwa anajitosheleza amekuwa akiendelea kuweka hadidu zake na wanaposhindwa kuzifuata anaendelea kupiga.

Hali imekuwa tete kwa nchi nyingi huku Afrika ikiumia zaidi kutokana na kuwa tegemezi kwa kiasi kikubwa, baadhi ya nchi zimeshatangaza njaa, kwa kushindwa kuingiza chakula kutoka Ukraine na Urusi, mafuta ndio kisanga kingine.

Bajeti ya Tanzania ya mwaka wa Fedha 2022/23 inaongezeko la 8% kutoka kwenye bajeti iliyotangulia, ongezeko hilo linaweza kuchangiwa sana na zoezi la sensa linalotarajiwa kufanywa mwezi Oktoba 2022.

Kutokana na uchumi kutokuwa vizuri na uwepo wa sintofahamu ya siku ambayo Urusi na Ukraine zitaacha mapigano, ni vyema hela ya sensa ikatumika kwa shughuli nyingine, ikiwemo kufinance shughuli za serikali na kutoa ruzuku kwa mafuta ili bei zibaki kuwa stable.

Zoezi la sensa ni muhimu lakini kwa uelekeo wa hali inaweza kuwa shida kwa serikali ambapo tunaweza kuta tunamatumizi makubwa ya kuhitaji kukopa zaidi wakati tunaweza kusubirisha baadhi ya matukio kama hili la sensa.

Zoezi lisubiri Uchumi utakaporudi katika hali ya kawaida, kwa sasa ni maumivu sana

Signed

OEDIPUS
 
Umeandika pumba we kilaza wa shule ya kata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…