Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kwema Wakuu,
Mimi ni mkaazi wa Kitongoji Kimoja wilaya ya Kinondoni hapa Dar es Salaam. Jumatatu nilipigiwa simu na watu wa TANESCO kunifahamisha kua Kwa kua number ya mita yangu inaanzia na 24... basi nitabadilishiwa mita hiyo kesho yake yaani juzi.
Juzi Jumanne kweli walikuja asubuhi kubadili wakanipa mita mpya. Mita waliyoitoa awali ilikua na units 56 lakini wao walinipa ya kwao yenye units 10 tu. Walisema hizo units 10 ni offer ya mita mpya lakin za awali hazipo tena. Huu ni utapeli wa wazi wazi. Ni uporaji na unyang'anyi waliojihalalishia, na hakuna uhalali wowote wa hili.
Baada ya kuweka mita mpya hiyo asubuhi wakaniambia watatuma number (token) za kufungulia hiyo mita. Nimesubiri mpaka usiku sijapata hiyo token, imekuja kutumwa jana mchana (zaidi ya masaa 24) Sina umeme, usumbufu ulioje. Waniibie units na umeme wasinipe.
Nimepokea token haifanyi kazi, kama vile ilikua wrong token. Customer Care ya TANESCO mmoja akasema kua inakua ngumu kutatua tatizo langu Kwa wakati sababu huu mradi hauko chini ya TANESCO moja Kwa moja, ni mradi wa mtu au kampuni binafsi. Yaani Ubabaifu uliopitiliza, watu wanajua mpaka number ya mita yangu lakin sio wa TANESCO .
Mpaka muda huu sina umeme kwangu toka juzi asubuhi (zaidi ya 40 hrs). Kama walikua hawajajipanga ni bora wangesitisha kwanza hili zoezi. Units mnazopora sio halali yenu kabisa, muangalie namna ya kutulipa.