Nyinyi ndio mnaendeleza watu kuibia serikaliWasiliana na diwani pamoja na mtendaji bila kusahahu mwenyekiti wa mtaa watakupa maelezo konki. Maoni yangu kama mtaa umeanza kuwa msafi haina shida, nataman hata huku wafanye hvo ili mtaa uwe Safi. Uchafu ni kero na kiukwel wanaosafisha inabd walipwe hela nzuri.
Kuna ubaya gani kama mtaa unakuwa msafi na taka wanazoa? Wakubwa wanapiga fedha hutaki na hawa wadogo nao wapate?Uwazi kwenye malipo ni muhimu, unaweza kufikiria unawalipa vizuri kumbe pesa inaishia kwa diwani na watendaji wachache.
NakaziaHebu jifunze kuandika vizuri, naona una hoja ,lakini kuna makosa ya kisarufi mengi tu.
Hebu tuliza mpira kiongozi.
Viatu vya mwenye kigoda wa kitaa au??Hela ya kubrush viatu!
Utoapo malipo dai risiti kinyume na hapo unawasaidia majizi kukuibia.tena ziwe za kielectronic.Habari wadau,
Kwenye mitaa yetu hususa huku uswazi kuna zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji 3000/= mpaka 5000/= kila kaya kiukweli hii ni pesa nyingi sana ambayo serikali za mitaa/mkandarasi wa taka anakusanya cha ajabu ukilipa haupewi risiti ya electronic.
Ila point yangu ni:
Je, hili zoezi limepata baraka zote toka wizara husika na serikali kuu?
Je, Taifa halioni linapoteza mapato kupitia utaratibu huu wa ukusanyaji na utoaji wa risiti zisizo za electronic?
Je, ushirikishwaji wa wananchi kuhusu viwango vya kulipia ulifuatwa?
Asanteni