Zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji Tshs 3,000 hadi 5,000 kila kaya bila kutoa risiti za kielektroniki lina baraka za mamlaka?

Zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji Tshs 3,000 hadi 5,000 kila kaya bila kutoa risiti za kielektroniki lina baraka za mamlaka?

Wasiliana na diwani pamoja na mtendaji bila kusahahu mwenyekiti wa mtaa watakupa maelezo konki. Maoni yangu kama mtaa umeanza kuwa msafi haina shida, nataman hata huku wafanye hvo ili mtaa uwe Safi. Uchafu ni kero na kiukwel wanaosafisha inabd walipwe hela nzuri.
Nyinyi ndio mnaendeleza watu kuibia serikali
 
Hao ni wezi kama wezi wengine tupaaze sauti yetu ifike kwa mh rais. Serikali ilipiga marufuku risiti za gerezani. Unaipotezea serikali mapato na nani alikuwambia diwani na mwenyekiti walipwe kwa kodi za taka?
 
Uwazi kwenye malipo ni muhimu, unaweza kufikiria unawalipa vizuri kumbe pesa inaishia kwa diwani na watendaji wachache.
Kuna ubaya gani kama mtaa unakuwa msafi na taka wanazoa? Wakubwa wanapiga fedha hutaki na hawa wadogo nao wapate?
 
Habari wadau,

Kwenye mitaa yetu hususa huku uswazi kuna zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji 3000/= mpaka 5000/= kila kaya kiukweli hii ni pesa nyingi sana ambayo serikali za mitaa/mkandarasi wa taka anakusanya cha ajabu ukilipa haupewi risiti ya electronic.

Ila point yangu ni:

Je, hili zoezi limepata baraka zote toka wizara husika na serikali kuu?

Je, Taifa halioni linapoteza mapato kupitia utaratibu huu wa ukusanyaji na utoaji wa risiti zisizo za electronic?

Je, ushirikishwaji wa wananchi kuhusu viwango vya kulipia ulifuatwa?

Asanteni
Utoapo malipo dai risiti kinyume na hapo unawasaidia majizi kukuibia.tena ziwe za kielectronic.
 
Huo utaratibu una baraka zote kutoka kwenye baraza la kata na mitaa yake..tatizo vikao vya wananchi vikiitishwa hamtokei kujadili haya..mwisho wasiku mnaishia kulaumu na kuhoji..chamsingi kesho j3 nenda katani au ofisi ya mtendajibwa mtaa akakupatie ufafanuzi.

Naamini utajibiwa vyema kuhusiana na suala zima la utoaji wa risiti.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom