micro_almunia
Senior Member
- Jan 16, 2011
- 134
- 37
UTANGULIZI:
Kwa muda sasa serikali imetangaza kuendelea na zoezi la urasimishaji ardhi kwa maeneo yasiyopimwa (squatters). Kufanikisha hilo, serikali imekuwa ikishirikiana na makampuni binafsi ya ardhi kufanya sehemu kubwa ya kazi hizo. Watu katika kampuni hizo wanalipwa kutoka kwa michango ya wananchi wa eneo husika ambako urasimishaji unafanywa.
Zifuatazo ni baadhi ya faida kubwa za kurasimisha ardhi:
i. Kuondokana na sehemu kubwa ya migogoro ya ardhi;
ii. Kuongezeka kwa mapato ya serikali ya kodi za ardhi na majengo
iii. Wamiliki wa ardhi kupata hati na hatimaye uwezo wa kutumia mali zao kama security kwenye taasisi za fedha; na kadhalika.
TATIZO/CHANGAMOTO:
Pamoja na faida lukuki zinazoambatana na zoezi la urasimishaji; speed ya mchakato imekuwa sio ya kuridhisha katika baadhi ya maeneo. Muda mwingi umekuwa ukitumika na kupelekea serikali na wananchi kuchelewa kunufaika na faida za kukamilika kwa mchakato huu. Changamoto kubwa (ambayo uzi huu umejikita) inayochelewesha na kusababisha kusua-sua kwa hili zoezi ni mwitikio usioridhisha wa baadhi ya wananchi katika kuchangia pesa ambazo ndio hutumika kuwalipa kampuni ama taasisi wanaofanya kazi.
MAONI ili kutatua Changamoto:
Nawasilisha hapa maoni kwenye Machaguo Matatu (Three Options) kwa serikali/wizara:
Option 1:
Serikali ipige hesabu ya viwanja vya kupimwa, imalizane kimalipo na kampuni zitakazopewa kufanya kazi maeneo husika. Ikiwa hivyo, kampuni zitalazimika kufanya kazi kwa muda bila kusua-sua na kukamilisha kwa ubora na wakati ili walipwe pesa zao zote (kulingana na idadi ya viwanja).
Baada ya hapo, serikali iweke ile gharama ya upimaji kwenye deni la kodi ya ardhi kwa viwanja husika. (Gharama ambayo ndio kile kiasi ambacho kwa sasa mwananchi hutakiwa kuchangia kulipa kampuni ya upimaji).
Hilo deni litakuwa litozwe interest/penalty baada ya muda wake wa kulipwa (grace period) kupita. Hiyo itahamasisha wamiliki wa ardhi kulipa kwa wakati na serikali kurudisha pesa zake ilizozilipa kwa kampuni za upimaji. Serikali pia inao uwezo wa kuzuia kutoa vibali vya ujenzi hadi pale ambapo kiwanja husika kitalipiwa gharama zake za upimaji.
Option 2:
Kama ilivyo option 1; badala ya serikali kulipa awali (ikiwa haitokuwa na fedha), inaweza kuingia mkataba na makampuni yatoyokuwa tayari; ambapo kampuni zitafanya kazi na baadae kuchukua pesa zitazolipwa na wananchi kama sehemu ya kodi zao za ardhi na majengo. Mikataba ieleze pia, mwananchi atapochelewa kulipa, pesa iongezewa riba (interest) ambayo nayo itakuwa halali ya kampuni waliopima. Serikali pia inao uwezo wa kuzuia kutoa vibali vya ujenzi hadi pale ambapo kiwanja husika kitalipiwa gharama zake za upimaji.
Option 3:
Serikali itumie wanafunzi walioko vyuo vya ardhi kufanya baadhi ya kazi halisi za urasimishaji wawapo kwenye mafunzo yao kwa vitendo (ikiwa inaruhusiwa kiutaratibu). Michoro ya hawa wanafunzi itahitajika kupitiwa kidogo tu na wataalamu wa wizara ili kufanyiwa maboresho kwenye mapungufu machache. Katika hilo, serikali itaokoa sehemu kubwa ya gharama na itaweza kukamilisha mchakato wa urasimishaji wa ardhi kwa gharama nafuu. Hapa pia gharama ndogo inaweza kuongezwa kwenye kodi za ardhi za viwanja husika kama option 1 na 2.
HITIMISHO
Kwa hali ilivyo sasa, hakuna hamasa ya kutosha ya kukamilisha zoezi la urasimishaji wa ardhi kwa speed itakikanayo. Makampuni hawako tayari kufanya kazi kwa sababu ya uchangiaji hafifu; na baadhi ya wanachi hawako tayari kuchangia kwa sababu, aidha hawataki kuanza kulipa kodi za ardhi ama hawana imani na mchakato kukamilika kwa wakati.
Ikiwa serikali itatumia 'advantage' waliyo nayo ya kuwa na mifumo imara pamoja na database zenye taarifa za wananchi; itaweza kuufanya mchakato ukaenda kwa haraka, ufanisi na mafanikio. Ndani ya muda mfupi, migogoro ya ardhi itapungua, kodi za ardhi na majengo zitakusanywa kwa wingi, na wanachi wengi zaidi wataweza kutumia ardhi zao kama security kwenye taasisi za kifedha.
Kwa ujumla, serikali indeleeni na kazi, ikamilike kwa wakati. Gharama nafuu za wananchi kuchangia ziwekwe kwenye kodi zao za ardhi.
Kanusho la Msingi kuhusu maoni hapo juu (Disclaimer):
Mtoa maoni sio mtaalamu wa ardhi, hajasoma maswala ya ardhi wala sheria za ardhi na pia hana uzoefu wowote wa kufanya kazi za ardhi. Maoni haya ni mawazo binafsi yaliyotegemea uelewa wa ujumla (general understanding) ya mtoa maoni. Msomaji asome zaidi kusudio na dhamira ya maoni haya na ikiwa ana mchango wa kitaalam zaidi autoe katika kuboresha.