wapendwa,
imani za wakristo wengi zimepoa kwa kutokuwa na kiasi kwao kwa mambo mbalimbali. mabinti ambao hawajaolewa na vijana ambao hawajaoa wamekuwa na bidii sana katika kusali na kufunga, lakini wanapooa/wanapoolewa, bidii yao hupungua na hatimaye hupotea kabisa. wengine husahau kabisa masuala ya kusali hadi wakati wa uzee wao ndio humrudia Mungu tena. moja ya sababu ya hali hii ni "kutokuwa na kiasi" katika "shughuli", malezi ya watoto, kutafuta pesa nk. na hivyo kumpa shetani fursa ya kuwatia majaribuni na kwa kuwa moyo hauna nguvu ya maombi, wamekuwa wakianguka kirahisi katika majaribu.
katika 1 Wakorintho 7:5 twasoma "msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali, mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu"
mi naona huyo mama yuko sahihi kama lengo lake ni kupata faragha ya sala na hicho alichoamua huyo mama kisingelaumiwa kama wangepatana na mumewe. wakristo tumeamuriwa kufanya kila jambo kwa kiasi ili tupate faragha kwa ajili ya sala. kwa kweli kwa kuwa na "shughuli" kila siku na kila wakati unapopatikana mwanya sio vyema kiimani na hata kiafya, ingawa sio dhambi.
ushauri wangu ni "kupatana" kama miezi mitatu ni mingi wapatane itakuwa kwa muda gani mwingine, na kama miezi mitatu ni michache pia wapatane. sie hatuna haki ya kuwaingilia bali ni wao na talanta zao walizopewa na Bwana.
Mungu wetu ni mkuu sana!
Glory to God!