"Nafahamu kwamba DPP amekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Massati, ambayo ilituachilia huru mimi na wenzangu tisa….hilo halinitishi.
"Nimewasilisha hati hiyo ya nia ya kutaka kuwashitaki na hawajanijibu, hivyo imeonyesha wazi wapo tayari kwenda mahakamani, na mimi na wakili tupo tayari na muda wowote kuanzia leo tunakwenda Mahakama Kuu kufungua kesi ya kudai sh bilioni tano ikiwa ni fidia ya usumbufu na kunyanyaswa kipindi kile nilipokuwa nakabiliwa na kesi ile ya mauaji.
"Sasa kitendo cha Jeshi la Polisi kunikamata na kunifikisha mahakamani na kwenda kuishi gerezani kwa miaka minne bila kuhojiwa na polisi, je, si ndiyo lilikiuka sheria na Katiba zilizotungwa na Bunge, ambapo na huyu huyu IGP aliapa kuilinda Katiba hiyo?" alihoji huku akionyesha kukerwa na jambo hilo.