Watanzania tutaendelea kulipa fidia hizi zinazotokana nauzembe wa watendaji na viongozi wa serikali mpaka lini? ukichukua hili suala la Zombe, huyu bwana alipona mkono wa sheria kutokana na sababu za kiufundi; hivi sasa serikali italazimika kumlipa mabilioni ya fedha za walipa kodi. Zipo fidia nyingi zinazulipwa kwa makondrasi wa barabara kwa uzembe kama huo. Leo serikali inadaiwa fidia nyingi zinazotokana na mikataba mibovu. La kushangaza ni kwamba wakati watanzania masikini wanalazimika kukosa matibabu na elimu kutokana na matumizi hayo mabaya ya raslimali ya taifa, wale wanaosababisha hasara hiyo wanaendelea kupeta.