Wakati wa kuondolewa madarakani DPP na kuvunja ofisi yake ili iundwe upya umefika. Maneno ya Zombe kuhusu ofisi hiyo kuwa na tabia ya kubambika kesi watu ovyo ovyo si ya kupuuzia maana yameshasemwa na wengi na kesi zingine zinafahamika kabisa.
Sasa kwa nini Raia wema waendelee kupata shida kwa ajili ya UPUMBAVU wa watumishi wachache ambao Raia haohao ndio wanawalipa?
Kupewa kesi ya kubambikwa kisha ukakaa Rumande kwa muda mrefu kwa ajili ya furaha ya mtu au makusudio binafsi ni kitendo kinachoumiza sana na kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Hawa watu waondolewe ofisi ile.