Zongo ni aina ya uchawi unaokaa machoni

Zongo ni aina ya uchawi unaokaa machoni

Ibun Sirin

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
50
Reaction score
106
Siku zote uchawi hauwaminiki uwepo wake au nguvu yake ispokuwa kwa wale waliodhurika nao.

Mwenye nao akikuangalia tu utaumwa tumbo hadi kufa, au akikiangalia chakula hata kipikweje hakiivi na kikiiva kinakuwa hakina ladha kabisa na watakaokila lazima matumbo yawaume sana halafu waharishe sana.

Zongo inaweza kupigwa kwa mtoto mchanga, mama mjamzito, n.k Zongo huwa ni Husda ya mchawi kwa kile unachokifanya au unacho jifagharisha nacho. Zongo inaweza kupigwa pia kwenye vyombo vya usafiri, kama umeshawahi kusikia gari hili limerogwa au kila wakati lina haribika na kutengenezwa, au kama umewahi kusikia boti hili linaharibika kila likipakia abiria au injini yake kufeli kila likipata mzigo wa kusafirisha.

Kujikomboa:
Dumu katika ibada, na pia Choma chumvi ya mawe nyumbani kwako na katika vyumba pia, huondoa sana nuksi katika nyumba, vyumba na sehemu ya bishara na katika vyombo vya usafiri.

1663580962514.png
 
Gharama kiasi gani mkuu ?
Uko serious ?
Maana unakuwaga mtu wa utani sana.
Siyo gharama sana mkurugenzi. Niandalie tu lita 1 ya mkojo wa paka. Usichanganyike na maji au kitu chochote.

Halafu uje na Jogoo 1 mkubwa bubu na asiyewika! Baada ya kupata hivyo vitu, nitakupa anuani ya kunifikia kwa urahisi..
 
Siyo gharama sana mkurugenzi. Niandalie tu lita 1 ya mkojo wa paka. Usichanganyike na maji au kitu chochote.

Halafu uje na Jogoo 1 mkubwa bubu na asiyewika! Baada ya kupata hivyo vitu, nitakupa anuani ya kunifikia kwa urahisi..
Nilijua kuwa uko na utani sana ngoja nianze kukusanya paka niwakojoleshe , kuku bubu sio shida ninaye hapa nyumbani

Ni jogoo ila sijawahi kumuona anawika
 
Je nawezaje kuwa mchawi ? Una njia za kunisaidia niwe mchawi ?
Mara nyingi uchawi unarithiwa, japo pia kuna uchawi wa kununua, lakini pia inategemea uchawi wa namna gani unauhitaji, kuna uchawi wa kuwanga, kujikinga, kuroga/kuagua watu, kufanya mazingaombwe, kujifurahisha, kudhuru watu n.k. Kwa vyovyote vile shart moja ni lazima kafara zihusike. Maeneo ambayo uchawi unaweza nunulika ni sehemu yoyote ile yenye vilinge vya uchawi.
 
siwezi sema moja kwa moja kama nimepigwa zongo lakin nahisi nina nuksi, ili kutoa zongo/nuksi hiyo chumvi ya mawe inachomwa vipi? kwa utaratibu upi?
Dah kweli kwa Yesu ni raha. Yaani nje huku kuna mahangaiko kweli kweli. Kuchoma chumvi tena?
Ndugu rudi kwa Mungu wako, Yesu ndio njia. Hautakuwa na haja ya kuchoma chumvi na mambo kama hayo.
Ukibarikiwa na Yesu hakuna wa kukulaani, awe shetani au vinyangara vyake.

Hakuna nuksi kwa mwana wa Mungu. Tafuta amani na Mungu wako na hutakuwa na haja ya kutahayari!
 
Back
Top Bottom