Zuchu achaguliwa tuzo ya Afrimma

Zuchu achaguliwa tuzo ya Afrimma

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Naona nyota ya huyu binti Ni Kali si mchezo tangu atambulishwe kwenye game haizidi hata miezi 6 ngoma zake alizoachia zimempa nominees kwenye tuzo za Afrimma kuania kwenye vipengele viwili Cha best Female East Africa na best new coming artist
 
Binti hana hata miezi sita.. kaanza kuwekwa matuzo ya africa.. huku kina ruby wana miaka na miaka hawawekwi... binti mitandaoni ma subscriber na ma followers kibao wakati katoka juzi juzi tu
 
Binti hana hata miezi sita.. kaanza kuwekwa matuzo ya africa.. huku kina ruby wana miaka na miaka hawawekwi... binti mitandaoni ma subscriber na ma followers kibao wakati katoka juzi juzi tu
Label inayomsimamia inajua nini inafanya...ni muda wake kujitengenezea njia ili huko mbele aje kujisimamia
 
Huyu msanii Kuna stage ameziruka atakuja kuzipitia baadae na majuto kibao wanaomsimamia wanamtengenezea bomu mbeleni

Hii sasa ndo tunaitaga 'roho ya uchawi'

Mzee baba umeanza kumjua Zuchu baada ya kutambulishwa rasmi na lebo yake na kuanza kuachiwa kwa nyimbo zake

Wala haujui ni kwa muda gani uyo Zuchu alikua anaandaliwa na kupikwa ipasavyo kabla hajawa released

Mkiambiwa WCB msanii anapikwa kwa zaidi ya mwaka mzima mnaona kama vile anaonewa na kucheleweshwa kutoa kazi zake, hayo sasa ndo matokeo ya kuandaliwa ipasavyo,ukapikika na ukaiva vilivyo!

Ondoa fikra potofu kama za mzazi mwenye uwezo mzuri tu wa kifedha na maisha safi,halafu mtoto wake anamsomesha kwenye shule za hali duni (kayumba) na kumpa maisha magumu,eti kisa tu kwakua uyo mzazi nayeye alipitia maisha hayo hayo magumu kabla ya kuwa na maisha mazuri.

Acha uchawi!!!
 
Kabla ya kutoka alikaa 4yrs benchi shida mnaangalia watu pale ulipoanza kuwajua na si kuangalia walipotokea.
Huyu msanii Kuna stage ameziruka atakuja kuzipitia baadae na majuto kibao wanaomsimamia wanamtengenezea bomu mbeleni
 
Tusio mpenda Zuchu ndo anazidi kutuchanganya zaidi.
Mfano mimi namuona zuchu kama vile ana sauti ya kuimba taarabu na umbea ila nashangaa anavyopaa?
Naunga mkojo hoja..
 
Kabla ya kutoka alikaa 4yrs benchi shida mnaangalia watu pale ulipoanza kuwajua na si kuangalia walipotokea.
Kwenye maisha kila kitu kina stage na hatua sasa Kama ana kasi hivi akifika mwaka si kashachuja tayari
 
Hii sasa ndo tunaitaga 'roho ya uchawi'

Mzee baba umeanza kumjua Zuchu baada ya kutambulishwa rasmi na lebo yake na kuanza kuachiwa kwa nyimbo zake

Wala haujui ni kwa muda gani uyo Zuchu alikua anaandaliwa na kupikwa ipasavyo kabla hajawa released

Mkiambiwa WCB msanii anapikwa kwa zaidi ya mwaka mzima mnaona kama vile anaonewa na kucheleweshwa kutoa kazi zake, hayo sasa ndo matokeo ya kuandaliwa ipasavyo,ukapikika na ukaiva vilivyo!

Ondoa fikra potofu kama za mzazi mwenye uwezo mzuri tu wa kifedha na maisha safi,halafu mtoto wake anamsomesha kwenye shule za hali duni (kayumba) na kumpa maisha magumu,eti kisa tu kwakua uyo mzazi nayeye alipitia maisha hayo hayo magumu kabla ya kuwa na maisha mazuri.

Acha uchawi!!!
Ulichoongea hakiendani na mada hongera kwa mjua zuchu toka yupo mdogo
 
Afrima hazijawahi kuwa tuzo zenye hadhi. Ni tuzo za kitapeli tu zenye madhumuni ya kibiashara zilizoanzishwa na wanaijeria.

Ndio maana wao nominees wanaangalia nani anakiki instagram.

Huo uhadhi wanauweka wabongo kwaajili ya kujivimbisha ili waonekane wako juu.

Afrimma naona wanatafuta fan base ila kwa sasa hawana reputation kubwa sana na wanajitahidi kuikamata East Africa ili kupata popularity. Labda baadae ndio zitakuwa kubwa
 
Back
Top Bottom