Hivi majuzi nilisikiliza
interview ya Sallam SK kupitia kipindi cha
The Switch cha Wasafi FM nikajifunza jambo -- kuwa kumbe si kila msanii yupo tayari kunyakua kila dili linalowekwa mezani, no matter how much mulla it brings.
Kumbe si ughaibuni tu ambapo watu wana uthubutu wa kukataa michongo ya pesa ndefu. Bongo tumefika pazuri. Inapendeza kuona sasa wasanii wetu wanaweza kuchagua pesa gani ya kuokota na ipi ya kuachia wengine.
Nimemsikia Mendez akisema bibiye Zuchu, kutokana na msimamo wake, hayupo tayari kukubali kazi za kutangaza vileo. Kwa mujibu wa meneja huyo, ambaye ninathubutu kumwita mwenye mafanikio zaidi kwenye soko la muziki wa Bongo, Zuchu could be pocketing big bucks from such endorsements.
Baada ya kufurahishwa na hayo, nimepata kujiuliza: msimamo huu unamaanisha pia kutofanya au kushiriki -- kwa namna yoyote ile -- kazi ambazo zinadhaminiwa na makampuni ya vileo? Vipi kuhusu matamasha yanayowezeshwa na vileo? Au hii ni yeye tu binafsi ndiye hataki kushika chupa na kutushawishi ni namna gani koo linasawijika linapokumbana na bia bariiiiiiid?
Natamani kufahamu msimamo wa Zuchu ni mpana kiasi gani. Ila kwakweli kuwa na misimamo ya namna hii mbele ya pesa ni jambo la kustahili pongezi.