Zuhura Yunus anazungumza na waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam, Juni 6, 2024

Zuhura Yunus anazungumza na waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam, Juni 6, 2024

Mimi ni kama kichuguu tu mbele ya Mheshimiwa Zuhura Yunusi ambaye ni kama Mlima Kilimanjaro. Mimi napenda sana kutambua uwezo wa mtu ,.sinaga wivu wala roho mbaya.ukiwa vyema katika eneo fulani la kazi huwa sioni haya wala aibu kukupa pongezi na heshima yako.
Poor you Lucas!!!
 
Sasa why mwanzoni hawakueleza haya mpaka wakurupushwe?
 
Mkutano wa kutetea uuzwaji wa eneo lenye madini ya kinywe Kwa wa Korea kusini ambao huo mkataba ni kichaa tu anayeweza kuukubali
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus pamoja na viongozi wengine wa Serikali wanazungumza na waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 6, 2024.


View: https://www.youtube.com/live/R29ql0qn41I?si=HUvsJC1La1-T6RWb
View attachment 3010105
View attachment 3010106
View attachment 3010107
View attachment 3010108
Viongozi mbalimbali pamoja na Waigizaji wakiwa kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu Mafanikio yaliyopatikana kufuatia Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea kuanzia tarehe 31 Mei, 2024 hadi tarehe 05 Juni, 2024.
View attachment 3010109
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea.
View attachment 3010111
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu masuala mbalimbali ya Teknolojia ya Mawasiliano wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali.
View attachment 3010112
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu, Dar es Salaam Juni 06, 2024 kuhusu masuala ya Uwekezaji wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea.


Yaani wazungumzaji wote hao .... Hapa ni lazima tUMEPIGWA. Inanikumbusha kipindi cha DPW ....!! Kwa nini Maza anatanguliza watu mbele wamsemee .... hivi yeye kama Kiongozi wa nchi hawezi kutetea maamuzi anayoyachukua ..!
 
Kwahiyo ikulu ya chamwino anaishi nani? Nawasiwasi litakuwa pagale
 
Bidada akaona afanye mkutano wake wa mwisho, akili mtu wangu
 
Imagine mafanikio makubwa kupatikana kwenye ziara ni KUKOPA...can you imagine!!!?
Halafu anakopa akizileta hapa nchini kuzisimamia vzr zisifisadiwe hawezi!
Hakika tumekula hasara kama Taifa
 
Kunifananisha Mimi na Mheshimiwa Zuhura Yunusi ni kumkosea pakubwa sana heshima na adabu Mheshimiwa Zuhura Yunusi.Ni kumdhalilisha na ni kumshushia heshima yake kubwa aliyojijengea ndani na nje ya Taifa letu na Duniani Kwote. Yaani mimi unilingaishe na Mh Zuhura aliyefanya kazi kwenye shirika kubwa La utangazaji la BBC? Embu acha dharau zako bwana hata kama ni utani basi huu umezidi pakubwa sana..mimi sina uwezo hata wa kusimama aliposimama Zuhura Yunusi. Ni sawa na kulinganisha mlima Kilimanjaro na tuta la karanga Mbozi huko.

Ningekuwa mimi ni Rais na nikataka kuteua Mkurugenzi Mkuu wa kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ikulu,kwa hakika bila kuchelewa ningemteua Mheshimiwa Zuhura Yunusi .kwa sababu anauwezo mkubwa ,uzoefu mkubwa katika Tasnia ya Habari tena kutoka chombo kikubwa kabisa cha habari hapa Duniani yaani BBC.

Lakini pia kama ingekuwa ni nafasi inapendekezwa halafu nikakuta tu jina langu lipo pamoja na la Mheshimiwa Zuhura Yunusi.basi mimi haraka sana ningejitoa na kumuachia nafasi hiyo Mheshimiwa Zuhura Yunusi. Hii ni kwa kuwa Zuhura ni Dada mwenye uwezo mkubwa,kipawa cha kipekee,ubunifu wa kipekee na Uwezo ambao sina wa kumfananisha naye hapa Nchini. Hivi unafikiri ni kazi nyepesi kupata kazi na mpaka akaaminiwa kuwa sehemu ya shirika la utangazaji la BBC Uingereza?

Kama ni viatu basi naweza kusema kiatu cha Mheshimiwa Zuhura Yunusi hakuna anayeweza kukivaa kikamtosha. Kwa kazi nzuri anayoifanya na Ubunifu wake wa kutoa mrejesho kila baada ya ziara ya Mheshimiwa Rais pamoja na mambo mengi ambayo amekuwa akifanya .Namuomba Mungu na Mheshimiwa Rais Aendelee kumuamini na kumuacha katika nafasi hiyo mpaka 2030. Na hata pia Atakaye kuja naamini hawezi kumuondoa Mheshimiwa Zuhura katika nafasi hiyo.

Naomba sana tuwe tunaheshimu Uwezo wa watu kuliko kuanza kuwadhalilisha kwa kuwafananisha na watu ambao ni Mbingu na ardhi.

Ungenjibu tu kwa mistari michache.

Sasa essay yote hii ya kazi gani?
 
Back
Top Bottom