Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
’Changamoto zitakuwepo lakini nitamudu kazi’’
Mkurugenzi wa mawasiliano ikulu nchini Tanzania, Zuhura Yunus amezungumza na BBC na kueleza ni jinsi gani amepokea taarifa ya uteuzi wake.
Kabla ya uteuzi huo bi Zuhura Yunus alikuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya Shirika la utangazaji la Uingereza BBC.
Bi Zuhura anachukua nafasi ya bwana Jaffar Haniu ambaye amepangiwa kuchukua majukumu mengine kulingana na Taarifa iliyotiwa Saini na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya rais.
-
Uteuzi wake unakuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.
Mkurugenzi mpya wa mawasiliano ikulu -Tanzania ameiambia BBC kuwa uteuzi wake ulikuwa wa kushitukiza na wala hakuwa na taarifa kama ameteuliwa kwenye nafasi ya kuwa msemaji wa ikulu!Anasema alikuwa amelala akashangaa simu za watu mbali mbali zinaita nakulia!
Anasema ni kitu ambacho hakutegemea kabisa!
Source: BBC Swahili