Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kawaida wataalamu wa afya wanaongozwa na maadili ya kazi, na inapotokea mtaalamu anakwenda kinyume na ethics za kazi sheria zinaelekezwa yeye kuadhibiwa na Mabaraza ya taaluma.Hawa wapumbavu wafutiwe tu usajili wa NHIF maana wanaongoza kuwapa watu wagonjwa wasiyokuwa nayo
Ni muhimu sana kujenga hoja mkuu. Tunajenga nchi mojaHuna lolote nyau wewe!
Upo sahihi mkuu hizo polyclinic nying wapigaji tuHawa wapumbavu wafutiwe tu usajili wa NHIF maana wanaongoza kuwapa watu wagonjwa wasiyokuwa nayo
Hoja muhimu ni kwamba huwezi kufuta au kuzuia huduma kwa sababu ya walio wachache ambao wanaweza kushughulikiwa na taratibu za kisheria.U
Upo sahihi mkuu hizo polyclinic nying wapigaji tu
Sio wapigaji tu bali wauaji wa binadamuU
Upo sahihi mkuu hizo polyclinic nying wapigaji tu
Naunga mkono hoja umeandika ukweli mtupu polyclinics nyingi zimekaa kiupigaji sana, NHIF Wana kazi kubwa ya kufanya kudhibiti wizi kwenye hivi vituo.Kwanini hizi Polyclinic hazitaki kutambua umuhimu wa Taaluma zingine kama Pharmacy na Wauguzi. Mamlaka zilinusa harufu ya uchafu uliokuwa ukifanwa na vituo hivi vya afya vitoavyo huduma za kibingwa. Udanganyifu na ukiukwaji wa taratibu katika kujaza fomu za bima kwa mfano, mnatumia MDs, AMO na maafisa Tabibu ila form wanajaza Madaktari bingwa. Hayo madudu yenu ndio yamepelekea mfumo wa bimq ya Taifa kushindwwa kujiendesha kwa kutumia mapato ya ndani.
Siungi mkono zuio, ila nalaani jeuri na kiburi mlichonacho Madaktari linapokuja suala la masuala ya sera za Afya. Ni vyema mkajitafajari ili Boss akija kuwaondolea zuio mnasonga. Ahsanteni sana kwa huduma zenu, zinahitajika nyingi sana bila ila acheni kiburi.
Wamejenga Benjamini Mkapa HospitalMfuko wa bima hauna Hela
Hela zimeenda wapi!? Wanasiasa wamwzichukua
Wanachi mfw tu
Hatari sana aisee.Wamejenga Benjamini Mkapa Hospital
Jumla ya pesa walizokopesha ni zaidi ya bilioni 400
Ila polyclinics ni maafa kwa binadamuHatari sana aisee.
Kumbe blanders ni za kwao wenyewe
Halafu wanatesa wananchi
Vijana wale wapi mkuu.Ila polyclinics ni maafa kwa binadamu
Kwa kifupi Polyclinics zilianzishwa kutokana na Sera zilizo chagizwa na NHIF, ambapo ilisababisha Vituo vingi kubadili hadhi kutoka dispensary, health center na kwenda Polyclinics.Vijana wale wapi mkuu.
Kuna majobless doctors Kila kona.
Hapo ndio wanakopatia ugali wao
Tunawashauri mje kwetu herbalists hatuna mbambamba tatizo dharau zenuHawa wapumbavu wafutiwe tu usajili wa NHIF maana wanaongoza kuwapa watu wagonjwa wasiyokuwa nayo
Hamna ukweli wowote wa hii habari.SINTOFAHAMU YA ZUIO LA USAJILI WA POLYCLINICS (KLINIKI ZA KIBINGWA) MPYA KATIKA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF): WAZIRI UMMY MWALIMU ATOE MAJIBU KWA WADAU
Kumekuwa na kilio cha Wadau katika sekta ya afya juu ya zuio la kusajili Vituo vya kutolea huduma maarufu kama Polyclinic na Specialized Polyclinic au Kliniki za Kibingwa katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, ambapo zuio hilo limelenga Kliniki mpya zilizoanza kutoa huduma mwanzoni mwa mwezi Aprili 2022.
Takwimu za Wizara ya Afya zinabainisha kwamba mpaka kufikia mwezi Machi 2022 kulikuwa na jumla ya Kliniki za Kibingwa 299 ambazo ni sawa na asilimia 3.3 tu ya vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Nchini.
Ni zaidi ya mwaka umepita bila kuwa na taarifa yeyote rasmi kutoka Wizara ya Afya kuhusu sababu za kutokusajiliwa kwa polyclinics mpya katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kutoa fursa kwa Watanzania kupata huduma bora bila kikwazo chochote, hasa ikizingatiwa Vituo hivyo vinaendeshwa kwa mujibu wa Sera na Miongozo ya Wizara husika, na pia zimekidhi vigezo stahiki.
Kwa mujibu wa chanzo cha Wizara ya Afya, zaidi ya Kliniki za Kibingwa 150 zimekwama kusajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya licha ya Vituo hivyo kukidhi vigezo vyote vilivyoainishwa na Mfuko na kwamba baadhi yake vilishafanyiwa tathmini ya vigezo na kuonekana kuwa na sifa za kusajiliwa ili kuhudumia wanufaika wa Mfuko huo, lakini kinyume na matarajio mchakato huo ulisitishwa bila taarifa yeyote kutoka kwa Mamlaka.
Baadhi ya Wawekezaji na Watoa huduma wamedai kwamba baada ya kukamilisha taratibu zote za maombi ya usajili wa Mfuko waliamua kufuatilia maombi yao kupitia Ofisi za Mfuko na kujulishwa kwamba kuna zuio kutoka Wizara ya Afya juu ya usajili wa Polyclinics katika Mfuko wa Bima ya Afya.
Wadau waliendelea kupaza sauti zao na kudai kwamba wanadhani Wizara ya Afya imeshindwa kutambua juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani kupitia sekta ya afya kwa kuweka zuio bila kutoa taarifa kwa wadau juu ya sababu zake na pengine zuio hilo linalenga kutatua nini, na litadumu kwa muda gani.
Kwa kukizingatia kwamba vituo vinategemea zaidi ya asilimia 70% ya mapato yatokanayo na wanufaika wa Mfumo wa Bima kwa ajili ya uendeshaji, ni wazi kwamba zuio hilo limeathiri kwa kiwango kikubwa uendeshaji wa vituo na kupelekea baadhi yao kusitisha huduma na wengine kuendelea kwa kusuasua.
Ni dhahiri kwamba zuio hili limeathiri uwekezaji na wawekezaji kwa kuwa uwepo wa Bima ya Afya na Uhaba wa huduma za Afya ilikuwa moja ya kivutio vilivyochochea uwekezaji katika sekta hii.
Inatajwa kwamba kiwango cha chini cha gharama za uendeshaji wa polyclinic moja zinakadiriwa kufikia Tsh. Milioni 10 kwa mwezi , ambapo kutokana na kukosekana kwa huduma ya NHIF vituo husika vimekuwa vikihudumia wagonjwa wasiozidi watatu (3) kwa siku licha ya Watanzania wengi kuendelea kupata adha ya msongamano wakati wa kupata huduma katika Vituo vilivyosajiliwa na Mfuko wa Bima ya Afya.
Aidha tathmini imebainisha kwamba katika kipindi chote cha zuio, Polyclinics zimehudumia wagonjwa kwa kiwango cha chini ya ufanisi unaokadiriwa kufikia asilimia 90-97% licha ya kutumia kiasi cha takribani Tsh. Bilioni 18 kwa mwaka kugharamia malipo ya mishahara, kodi ya pango, kodi za kimamlaka na gharama nyingine za uendeshaji, ambapo gharama hii ni nje ya ile iliyotumika kufanya uwekezaji.
Kuendelea kwa zuio hili, inaweza kupelekea takribani Watanzania wasiopungua kumi (10) kwa kila polyclinic kupoteza ajira zao pale ambapo Vituo vitasitisha kutoa huduma, na hivyo kutengeneza ukosefu wa ajira wa takribani watumishi 1500, kiwango ambacho ni kikubwa sana ukizingatia hali ya upatikanaji wa ajira na changamoto zake.
Zaidi, imethibitika kwamba zuio hili linawanyima wanachama wa Mfuko wa NHIF fursa ya kupata huduma bora, za kibingwa , kitendo ambacho ni kinyume na sera na jitihada za serikali kuhakikisha huduma bora zinafikia wananchi.
Ni matumaini yetu kwamba uwepo wa Vituo vingi vya kutolea huduma za Afya Mathalani Kliniki za Kibingwa ambazo zimesajiliwa na Mfuko wa NHIF itakuwa ni fursa kwa Mfuko katika kuboresha huduma kwa wanachama wake, na hivyo kuvutia Makundi mengi zaidi kujiunga, na hatimaye Ukuaji wake.
Uwepo wa huduma bora, na za uhakika kwa Wananchi utasaidia kufanikisha adhma ya Serikali ya kuwa na Bima ya Afya kwa Wote.
Hivyo basi tunatoa wito kwa Wizara ya Afya kuingilia kati ili kunusuru hali hii mbaya, na hivyo kuinua hari na matumaini kwa wawekezaji wazawa, watumishi wa sekta ya afya na wananchi kwa ujumla.