Zulia vs Kapeti, kipi kinafaa kwa geto?

Zulia vs Kapeti, kipi kinafaa kwa geto?

Beberu

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2017
Posts
4,548
Reaction score
9,740
Wakuu, hiv kipi kipo poa kwa geto? Kati ya zulia au kapet la manyoya?

Zulia.

IMG-20240403-WA0033.jpg

Kapeti za manyoya
IMG_20240403_200013.jpg
 
Wakuu, hiv kipi kipo poa kwa geto? Kati ya zulia au kapet la manyoya?

Zulia.

View attachment 2953113
Kapeti za manyoya
View attachment 2953111
Vyote ni vizuri iwapo vitawekwa sehemu sahihi.Kwa mfano hilo la nyuzinyuzi hufaa zaidi sehemu isiyo na pilikapilika na yenye kudumisha usafi(vumbi na tope ni adui).Usafishaji wake ni wa gharama, huchukua muda na nguvu nyingi.Ghrama kununua.

Hilo lingine la nylon(lailoni?)utunzaji wake ni mwepesi ila huchakaa haraka kulingana na lilipowekwa kimatumizi na watumiaji wenyewe.Siyo gharama sana kununua.
 
Kuna tofauti kati ya zulia na kapeti (carpet)? Mimi nadhani zulia ni kiswahili cha neno carpet!!!!!!!!!
Kuna mtangazaji wa TBC redio alisikika akisema msafara utatoka uwanja wa taifa utapita barabara ya Nyerere Road, kama haitoshi akasema watakwenda mpaka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere International Airport
 
Vyote ni vizuri iwapo vitawekwa sehemu sahihi.Kwa mfano hilo la nyuzinyuzi hufaa zaidi sehemu isiyo na pilikapilika na yenye kudumisha usafi(vumbi na tope ni adui).Usafishaji wake ni wa gharama,huchukua muda na nguvu nyingi.Ghrama kununua.
Hilo lingine la nylon(lailoni?)utunzaji wake ni mwepesi ila huchakaa haraka kulingana na lilipowekwa kimatumizi na watumiaji wenyewe.Siyo gharama sana kununua.
Ahsante kwa ufafanuzi mzuri
 
Ukisema carpet kule uswahilini tunajua ni yale ya draft ya plastic..ukiweka kwenye nyumba yanaharibu sakafu!..haya mazulia ndio ya kisasa hasa..japo nayahitaji ustaarabu sana..chukua zulia la manyoya ila halitaki movement nyingi.
 
Kuna watu wana jeuri hata walikute hilo la manyoya wanaingia na viatu vyenye tope
Mengine unasamehe tu.Uchague moja kati ya;-

- Mgeni avue viatu na soksi mlangoni ushuhudie miguu(kwato)ilivyopauka,kuchanika ugwambala,magaga,makenya kama amekula simenti?

- Mgeni avue viatu abakize soksi zilizochanika adhalilike na kueneza harufu kali ya uvundo (kuoza?)wa miguu na soksi?

Chagua lenye afadhali.
 
Hili ni chaguo la mtu hasa ikitegemea upo sehemu gani na nyumba inaingia watu gani na kwa kiasi gani. Kapeti la manyoya kama sehemu ina viroboto utakoma. Kwa kifupi lenye manyoya linahitaji nyumba nzuri za kistaarabu.
Lipi linapendezesha geto zaidi ?
 
Back
Top Bottom