Zumaridi na wenzake wakutwa na kesi ya kujibu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imewakuta na kesi ya kujibu, Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi na wenzake nane katika mashtaka matatu yanayowakabili.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya Jinai namba 12/2022 ni Zumaridi, Amos Kailembo, Isaya John, Isaka Mafuru, Neema Julian, Suzana Simon, Anitha Yesaya, George Maloji na Veronica Emmanuel.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Oktoba 4, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Monica Ndyekobora wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo washtakiwa hao wanakesi ya kujibu au laa.

Zumaridi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kufanya shambulio la kudhuru mwili, kuzuia askari kutekeleza majukumu yake na kuzuia ofisa wa umma kutekeleza majukumu yake.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, Februari 23 mwaka huu nyumbani kwa Zumaridi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa jijini Mwanza kinyume na kifungu namba 241, 243 (b) na 114 (a) na (b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Hakimu Ndyekobora amesema mahakama imewakuta washtakiwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa mashahidi 12 na vielelezo 11.

Baada ya kutamka hivyo akawataka mashahidi kusema watajitetea kwa kiapo au bila kiapo ambapo wakili wa Utetezi, Steven Kitale amesimama na kuieleza mahakama kuwa washtakiwa wote watajitetea kwa kiapo.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu, Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo huku akisema ushahidi wa upande wa utetezi utasikilizwa kwa siku tano mfululizo kuanzia Oktoba 17 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
 
Naona milango ya gereza la Butimba inaanza kufunguka polepole ili kuruhusu Zumaridi na wenzake kuchoma ndani. Mara nyingi Mahakama ikisema mtu ana kesi ya kujibu hawezi shinda kamwe
 
Ila sas kosa analofungwa nae siyo la kutishia uai wa mtu nadhani kuna kitu amewaudhi watawala hyo kesi nyepesi sioni kesi Happ

Bora ingekuwa Ni kuuidharau mahakama

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Akiingia Butimba atakua Zuma halisi cheusi mangara,labda wawe wanampenyezea cream na maji yake ili amaintain rangi
 
kesi ishakua nyepesi kumbe sio kama tukivoambiwa wamekutwa na wahamiaji haramu ...
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imewakuta na kesi ya kujibu, Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi na wenzake nane katika mashtaka matatu yanayowakabili.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya Jinai namba 12/2022 ni Zumaridi, Amos Kailembo, Isaya John, Isaka Mafuru, Neema Julian, Suzana Simon, Anitha Yesaya, George Maloji na Veronica Emmanuel.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Oktoba 4, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Monica Ndyekobora wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo washtakiwa hao wanakesi ya kujibu au laa.

Zumaridi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kufanya shambulio la kudhuru mwili, kuzuia askari kutekeleza majukumu yake na kuzuia ofisa wa umma kutekeleza majukumu yake.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, Februari 23 mwaka huu nyumbani kwa Zumaridi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa jijini Mwanza kinyume na kifungu namba 241, 243 (b) na 114 (a) na (b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Hakimu Ndyekobora amesema mahakama imewakuta washtakiwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa mashahidi 12 na vielelezo 11.

Baada ya kutamka hivyo akawataka mashahidi kusema watajitetea kwa kiapo au bila kiapo ambapo wakili wa Utetezi, Steven Kitale amesimama na kuieleza mahakama kuwa washtakiwa wote watajitetea kwa kiapo.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu, Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo huku akisema ushahidi wa upande wa utetezi utasikilizwa kwa siku tano mfululizo kuanzia Oktoba 17 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
Tawileeee maisha mema mfalme wetu uko gerezani
 
Naona milango ya gereza la Butimba inaanza kufunguka polepole ili kuruhusu Zumaridi na wenzake kuchoma ndani. Mara nyingi Mahakama ikisema mtu ana kesi ya kujibu hawezi shinda kamwe
Hapana, haipo hivyo mkuu,

Hapo na wao wataleta ushaidi wao na mashaidi wao, na pia watapewa nafasi ya kuwahoji mashaidi upande wa jamuhuri hili mahakama ipate kutambua ukweli ni upi
 
Back
Top Bottom