Zungu achana na tozo hangaika na Liganga na Mchuchuma

Zungu achana na tozo hangaika na Liganga na Mchuchuma

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mbona unayalaumu mabenki na makampuni ya simu, Kwani serikali haitozi kodi kwenye miamala inayotoza mabenki na makampuni ya simu kwa watumiaji? Yaani Mh. Zungu unachotaka wewe ni serikali akate kodi kwenye makusanyo ya mabenki na makampuni ya simu kutoka kwa mteja halafu mkate kodi tena kwa mteja huyohuyo tena aliyekatwa na makampuni ya simu na mabenki kwenye muamala huohuo.

Yaani kule kwa kampuni unachukua halafu huku kwangu unachukua tena kwa muamala huohuo mmoja. Hii sio sawa, na kama unadhani mabenki na makampuni ya simu yanawatoza wananchi pesa nyingi sana kwanini serikali isiyakate kodi kubwa pia kwa kila mwamala na kuachana na wananchi? Maana kama TRA ikisema kila mapato ya miamala ya mabenki na makampuni ya simu wataka 30% ingetosha kupata hela hukohuko kwenye mabenki na makampuni ya simu na kuachana na tozo kutoka kwetu.

Lakini kuna fedha nyingi huko bandarini, mkongo, usafirishaji, baharini, kwenye gesi na kwenye makaa ya mawe na madini ya chuma huko Liganga na mchuchuma kwani bunge lisijielekeze zaidi kwenye kuvuna hela kutoka huko? weledi uko wapi? Tozo tozo kila wakati, khaaaaa!

Hio liganga hadi ianze kuzalisha si watakuwa hawapo madarakani, wao wanaangalia kipi cha haraka cha kupiga thus wanapenda kukopa na tozzo. Kama ni ishu ya kupata pesa vipo vyanzo vingi Sana na pesa nyingi Sana bila kuwakamua watu masikini kodi.
 
Magufuli alianza kujenga reli kabla ya kujenga kiwanda cha chuma.
 
Yaani sisi ni takataka kabisa hivi unaweza kweli ukajiita kiongozi na una amani kabisa huku watu wako unaowaongoza wanateswa na umasikini.
Unashindwa vipi kuufuta umasikini huku una KILA kitu.
Ardhi, pesa, Nguvu Kazi, masoko, nk
 
Samaki wako wengi baharini lakini Zungu anashindwa kuiambia serikali tutawavua vipi tupate mapesa, anang'ang'ana na tozo kwa walalahoi. Kaama mabeki wanatoza waananchi pesa nyingi si aende huko akayakate kodi kubwa? Yaani anataka akate kwenye makampuni na kwetu pia, yaani tukatwe mara mbili sisi.
 
Hovyo sana wamemtuma wenzake Hakuna jambo linaloweza pendekezwa bila wao kukaa
 
Zungu ana elimu gani huyu jamaa
Kaishia form two Azania.
Kauza sana ngada hapo Ilala.
Kisha akachukua kadi ya CCM na kadi ya uanachama wa Simba...

Mara paap ubunge...Mara paaap unaibu Spika.

Ujanja ujanja tu hapo uliza elimu atakuonyesha hata vyeti vya Harvard, ubashite mtupu.
 
Ndo maana mawazo yake uendana elimu yake.
 
Back
Top Bottom