Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hana huruma na watanzania hata kidogo, ametuua kwa ngada sasa hivi anataka kutuua kwa tozo.Ndo maana mawazo yake uendana elimu yake.
Huyu mzee hivi anajuwa wengi wetu tukiamka ndiyo tunawaza hela ya mboga tutapata wapi? mana kipato chetu hakiruhusu kulala na akiba.Hakika aliyeshiba hamjuwi mwenye njaa.Mbona unayalaumu mabenki na makampuni ya simu, Kwani serikali haitozi kodi kwenye miamala inayotoza mabenki na makampuni ya simu kwa watumiaji? Yaani Mh. Zungu unachotaka wewe ni serikali akate kodi kwenye makusanyo ya mabenki na makampuni ya simu kutoka kwa mteja halafu mkate kodi tena kwa mteja huyohuyo tena aliyekatwa na makampuni ya simu na mabenki kwenye muamala huohuo.
Yaani kule kwa kampuni unachukua halafu huku kwangu unachukua tena kwa muamala huohuo mmoja. Hii sio sawa, na kama unadhani mabenki na makampuni ya simu yanawatoza wananchi pesa nyingi sana kwanini serikali isiyakate kodi kubwa pia kwa kila mwamala na kuachana na wananchi? Maana kama TRA ikisema kila mapato ya miamala ya mabenki na makampuni ya simu wataka 30% ingetosha kupata hela hukohuko kwenye mabenki na makampuni ya simu na kuachana na tozo kutoka kwetu.
Lakini kuna fedha nyingi huko bandarini, mkongo, usafirishaji, baharini, kwenye gesi na kwenye makaa ya mawe na madini ya chuma huko Liganga na mchuchuma kwani bunge lisijielekeze zaidi kwenye kuvuna hela kutoka huko? weledi uko wapi? Tozo tozo kila wakati, khaaaaa!