Japo ni kweli Mhe. Ado alifanya utovu wa nidhamu kuendelea kuongea hata baada ya kuzimiwa mike, lakini kiukweli na kihaki, kanuni hiyo ya 85 ina makosa ya upungufu wa haki, na kuutetea udikiteta wa Spika wa Bunge!.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, Spika wa Bunge ni bonge la Dikiteta, akisema nyamaza! kaa chini!, unapaswa kukaa chini!.
Kanuni hii
View attachment 3577325
Ina makosa ya ki haki.
Kama muda wa mbunge kuchangia ni dakika 10, kunapotokea, mbuge akakatizwa kuhusu utaratibu, au taarifa, Spika anatakiwa kuulinda muda wa mchangiaji ulioliwa na kuhusu utaratibu au taarifa !.
Mimi ni mmoja wa watu tuliofuatilia mjadala huu, muda wa Mhe. Ado kuchangia, uliliwa sana na taarifa za taarifa, na baada ya taarifa ya mwisho, muda rasmi wa Mhe. Ado, ukawa umekwishwa bila kufidia ule muda wake wote uliomegwa na watoa taarifa!.
Ili kuiboresha hii kanuni na kuifanya ya haki, ibara ya
80.-(1) Mbunge yeyote anaweza kusimama mahali pake na kusema na kwa ruhusa ya Spika, atatoa taarifa au ufafanuzi kwa muda wa dakika zisizozidi mbili kwa Mbunge anayesema, ambapo Spika atamtaka Mbunge anayesema aketi kusikiliza taarifa hiyo.
(2) Mtoa taarifa atakapomaliza kutoa taarifa na kuketi, Spika atamuuliza Mbunge aliyekuwa akisema mwanzo kama anaikubali au haikubali taarifa hiyo kabla ya kumruhusu kuendelea kuchangia hoja.
inatakiwa kuongezewa
(3) Spika ataulinda muda wa mbunge, ulioliwa na watoa taarifa, kwa kumfidia, achangie kwa muda mrefu zaidi ili kutimiza muda wake wa uchangiaji.
Jambo kama hili liliwahi kujitokeza kule nyuma Mhe. Zungu akiwa Naibu Spika, niliwashauri wabunge
Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika! na nilimpongeza
Vicky Kamata Anastahili Pongezi! Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu!
Mhe. Ado Shaibu ni mtu sahihi wa kusimamia haya madudu kuondoshwa kwenye Bunge letu!.
P