Zungu: Bando likibaki lisikatwe, lihamishiwe kwenye kifurushi kipya

Zungu: Bando likibaki lisikatwe, lihamishiwe kwenye kifurushi kipya

Bunge linakosea.

Iwe hivi

Nimenunua kifurushi sijatumia basi iwe sijatumia. Muda usiamue kifurushi kuisha bali matumizi ndiyo yaamue kifurushi kuisha
 
Nchi nyingi bando likibaki linapelekwa kwenye kifurushi kinachofuata, na hapa iwe hivyo bando likibaki lisikatwe lipelekwe kifurushi kinachofuata.

Unaweza kuona sh, 50 inayobaki kwa watu milioni 20 kwa kila bando ambayo inaliwa ni kama bilioni moja ambayo inabaki kwenye kampuni za simu, bando lisikatwe liachwe mpaka liishe kwa mteja mwenyewe.

Pia soma: Shigongo: Kuna vilio vingi kuhusu mabando ya simu, TCRA CCC isimamie, Wananchi wananung’unika
Halotel waliwahi kufanya, lakini fisadi Nape akawazindua wakaondoa.
 
sasa ushalipia kifurushi kwa ajili ya wiki au mwezi ukibakisha dakika au Mb mwenyewe ufanyiwe huruma ya nini? wabongo tunapenda mteremko kupindukia
Tuliza akili jiulize:
ukinunua kitu kwa mtu, ukakitumia kikabakia, unastahili kunyang'anywa na mtu yule yule aliyekuuzia?

Au waweza kukiweka ukakitumia baadaye ama kukigawa kwa mwingine kwa sababu ni haki yako?
Bado na jiuliza na hili la kununua line, usipoitumia miezi3 wakunyang'anya.

Je ni haki kupokonya mali ya mtu aliyouziwa kihalali?

WaT tushaonwa wajinga sana.
 
Back
Top Bottom