Zungu: Dar Maji hamna, lakini bili zinakuja kama kawaida shida ni nini?

Zungu: Dar Maji hamna, lakini bili zinakuja kama kawaida shida ni nini?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Spika wa Bunge, Mussa Zungu ameitaka Wizara ya Maji kufuatilia sababu za kuendelea kutolewa bili za maji kwa wakazi wa Dar es Salaam licha ya kuwapo kwa uhaba mkubwa wa maji kwa kipindi kirefu.

Akizungumza leo Jumatano, Januari 28, 2026, bungeni jijini Dodoma, Zungu amesema hali hiyo ni kero kwa wananchi na inahitaji hatua za haraka.

"Kulikuwa na uhaba mkubwa sana wa maji Dar es Salaam lakini bili zinaendelea kuja kama kawaida. Shida ni nini? Kalifanyie kazi,” amehoji Zungu.

 
Mimi naishi Kiluvya Madukani na sijapata issue ya kuletewa bill pasipo kupata hudumai. Kwa kweli siungi mkono hoja ya Babu Zungu. Hiyo changamoto haipo kwa kila mkazi wa DSM
 
Back
Top Bottom