Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (Mb), Juni 15, 2026, ameeleza Bungeni kuwa tangu Serikali ilipofanya marekebisho ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOKA) mwaka 2016, kampuni zote za simu zilitakiwa kuuza angalau asilimia 25 ya hisa zake kwa umma kupitia soko la hisa ndani ya kipindi kilichoishia Juni 2018.
Amesema hadi sasa ni kampuni ya Vodacom pekee iliyotekeleza takwa hilo la kisheria, huku akihoji kwa nini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) zimeshindwa kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa na kampuni nyingine.
Soma: Fahamu Faida na Mbinu za Kupeleka Kampuni/ Biashara katika SOKO la HISA
Kutokana na hali hiyo, Spika amezielekeza TCRA na CMSA kukutana na Kamati ya Bajeti kueleza sababu za kutotekelezwa kwa sheria hiyo, akisisitiza kuwa Serikali inapoteza mapato mengi kutokana na kutotekelezwa kwa sheria, huku akitolea mfano nchi jirani inayokusanya zaidi ya Shilingi bilioni 480 kwa mwaka kupitia gawio la kampuni za simu.