Zuwena wa Diamond Platinum ni nani kiuhalisia?

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,354
Reaction score
4,024
Umuofia kwenu,

Igweeeeeee.

Shwari wapenzi wana JF.

Your browser is not able to display this video.

Naomba ku-declare interest kwamba mimi ni shabiki kindaki-ndaki wa Diamond Platinumz.

Kulingana na uhalisia wa jamii tunamoishi, nimejikuta nautafakari sana wimbo wa Zuwena ambao gwiji huyu wa bongo fleva aliuachia muda si mrefu.

Mwanzoni sikumwelewa Diamond zaidi ya kumshangaa kaimba nini!

Lakini kadri siku zinavyoendelea, napata ka-mwanga kidogo kuhusiana na ujumbe ambao 'dogo' alitaka kuufikisha kwa hadhira.

Kwa ambao hamjawahi kuusikiliza, wimbo wa Zuwena ni kisa cha mjane ambaye alianza kufuja mali za urithi alizoachiwa na kufanya mambo ya hovyo hadi kugeuka kuwa kituko na kutia aibu kubwa sana kwa familia na jamii yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…