JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

TAARIFA KWA WANACHAMA, WANANCHI NA WAPENZI WA CHADEMA TANZANIA Ndugu wanachama, Wananchi na wapenzi wa CHADEMA, Tunapenda kuwajulisha kuwa tarehe ya uzinduzi wa Operation #NoReforms, NoElection – Kanda ya Nyasa (Mbeya) imebadilishwa kutoka 23 Machi 2025 hadi 1 Aprili 2025. Marekebisho haya yamefanywa kutokana na sababu za kifedha na maandalizi yanayohitaji muda wa ziada ili kuhakikisha uzinduzi unafanyika kwa mafanikio makubwa na kwa ufanisi wa hali ya juu. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na tunawashukuru kwa uvumilivu wenu. Tunaendelea kuwasihi muendelee kuwa na hamasa, mshikamano, na utayari kwa siku hiyo muhimu. Kamati ya Maandalizi: Operation No Reforms, NoElection Kanda ya Nyasa - Mbeya.
LISSU KWENYE UKURASA WAKE WA X (TWITTER) AMENENA MAZITO ASEMA HATA AKIBAKI MWENYEWE CHADEMA ITASONGA. Hayo yamekuja mara baada ya viongozi mbalimbali wa Kanda wa CHADEMA kujiuzulu kwa madai ya Chama chao (CHADEMA) kukosa Muelekeo na Kwenda kujiunga na ACT wazalendo ili kuongeza nguvu kwenye chama chenye nia ya mabadiriko ya kweli sio kwa Sasa CHADEMA imejifia kifo cha asili sema viongozi taifa hawataki kusema ukweli.
Wakuu hii taarifa nimekutana nayo Facebook je, ni ya kweli? 𝐁𝐎𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐈 𝐊𝐔𝐉𝐈𝐔𝐙𝐔𝐋𝐔 𝐍𝐀𝐅𝐀𝐒𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐄𝐍𝐘𝐄𝐊𝐈𝐓𝐈 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐊𝐀𝐍𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈 Habari za ndani kabisa ya CHADEMA zinasema bundi ameendelea kulia; safari hii Boni Yai akitajwa kuwa mbioni kujiuzulu kutoka nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani, na kwamba barua yake ya kujiuzulu tayari ameshaiwasilisha kwa Katibu Mkuu John Mnyika. Hatua hii inatokana na kutokukubaliana na uongozi mbovu wa Tundu Lissu na migogoro inayoendelea ndani ya chama hicho. Kujiuzulu kwa Boni Yai kunadhihirisha mpasuko mkali ndani ya CHADEMA, huku migawanyiko ya kimtazamo ikizidi kuleta mvutano mkubwa kati ya wanachama na viongozi wa juu wa chama.
Ndugu zangu Watanzania, Unaweza kusema ya kuwa Mheshimiwa Boniface Jacob ameamua kujiweka pembeni ya ulingo na masuala mazima ya siasa za CHADEMA na kuamua kujikita kwenye shughuli zake binafsi za kijasiriamali. Ambapo Mheshimiwa Jacob ambaye ni Mayor wa zamani wa Ubungo ameonekana akiwa katika chumba au ukumbi wenye Trei za mayai Mengi sana. ambayo ni biashara amekuwa akiifanya kwa muda mrefu sana na ambayo imeonekana kumpatia matokeo chanya na faida kubwa sana. Amepongezwa sana mitandaoni na watu mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti kwa juhudi zake kubwa na kuwa mfano wa Kuigwa katika mapambano ya kukabiliana na umaskini na kujikwamua kiuchumi. Wengi wamemsifu na kusema kwa hakika anapaswa kupewa sapoti na kuungwa mkono sana...
Back
Top Bottom