PreGE2025 POTOSHI Viongozi wa CHADEMA wamekiri kushindwa Uchaguzi, waogopa, wakubali ushindi wa kishindo CCM

PreGE2025 POTOSHI Viongozi wa CHADEMA wamekiri kushindwa Uchaguzi, waogopa, wakubali ushindi wa kishindo CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Wakuu

Je, Ni kweli viongozi wa CHADEMA wamekiri kushindwa Uchaguzi, waogopa, wakubali ushindi wa kishindo CCM
1742558524963.png

 
Tunachokijua
Mnamo Machi 08, 2025 Baraza la Wanawake la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, BAWACHA liliadhimisha siku ya wanawake duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu.

Kutokana na hotuba aliyokuwa ameitoa Lissu katika maadhimisho hayo, kumeibuka video inayojumuisha viongozi wengine wa CHADEMA kuwa wamekiri kushindwa uchaguzi, kuogopa na kukubali ushindi wa CCM.


Uhalisia kwa Kipande cha Video kinachomuhusisha Lissu

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kwa kuhaririwa, ikikatwa vipande vidogovidogo kutoka kwenye hotuba ya Lissu iliyorushwa mbashara na Jambo TV, na kuviunganisha hivyo kutengeneza maana tofauti. Tazama video halisi hapa kuanzia 6:20:51 ambapo Lissu alisema,

Hata hivyo Lissu hakusema kama anaogopa uchaguzi bali alihoji wanaosema anaogopa uchaguzi akibainisha kuwa yeye ni miongoni wanaopenda bunge na awali aliwahi kugombea na kushinda huku kwa sasa akisema ni lazima mazingira mazuri yaatengenezwe ili kuimarisha uwazi katika uchaguzi.

"Hivi nani anayeweza kusema mimi naogopa uchaguzi, mimi niligombea ubunge na miaka 27 nimetoka chuoni mwaka 1995 nikachaguliwa mara mbili, kama ni utamu wa ubunge naufahamu. Kwahiyo Swala la kwamba naogopa uchaguzi, kuna mtu anayependa bunge kama mimi? sasa hivi haiwezekani tena wale wanaofikiria twende tu twende tu, tutengeneze mazingira mazuri ya chaguzi ili twende uchaguzi uchaguzi tukijua tukipigiwa kura, kura za watu wetu zitahesabiwa na zitahesabika."

Aidha Tundu Lissu alieleza namna ambavyo mfumo wa uchaguzi unahitaji kufanyiwa mabadiliko kwani mfumo huo umetawaliwa na chama tawala huku akibainisha kuwa namna pekee ya kubadilisha siasa na serikali ni kupitia uchaguzi.

"katika nchi yetu namna pekee ambayo ni halali ya kubadilisha siasa ni kwa kufanya uchaguzi, namna inayoruhusiwa kubadilisha serikali kwa utaratibu wa nchi hii wa kikatiba ni uchaguzi, kama hiyo ndiyo namna pekee inayoruhusiwa, then suala la mfumo wa uchaguzi ukoje ni suala la msingi kwelikweli, tunachaguanaje ni suala la msingi kuliko suala lingine lolote kwa sabababu ndilo linalotuonesha kama kuna uwezzekano wa kubadilisha siasa za nchi hii, wa kubadilisha uongozi wa nchi hii"

"Tume ya uchaguzi, mfumo wetu wote wa uchaguzi ni mfumo wa CCM. Sasa tuulizane kwenye huo mfumo wa CCM Tunatoboa? hatuwezi tukatoboa..."



Uhalisia wa kipande cha video kinachomuhusisha John Heche


Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa kipande hicho cha video kimepotoshwa kutokana na kukatwa hivyo kutokukamilika kwa sehemu hiyo ya mazungumzo. Aidha Chanzo cha video hiyo ni mahojiano aliyofanyiwa Heche katika kipindi cha Super Breakfast cha East Africa Radio ambapo sehemu ya video hiyo baada ya kuulizwa kama wanafikiria kuhusu mgombea kuelekea uchaguzi mkuu Heche alisema,

"No Reforms No Election, Juzi nilimsikia Makalla anasema hivi, hatujajiandaa, hatuna fedha. Uchaguzi sio fedha mimi nilishinda udiwani natembea kwa mguu, niligombea na mtu anaitwa Peter Zacharia 'a multi-billionaire' ana mabasi kanda ya ziwa nzima kama Abood nikamshinda na nilikuwa mwanafunzi, nimeenda kwenye ubunge sina hata gari nikashinda ubunge"


Kipande cha video kilichomuhusisha Mwenyekiti wa baraza la wanawake kanda ya Serengeti Rosemary Kirigini


Ufuatiliaji wa JamiiCheck ulibaini kuwa kipande hicho cha video kilikatwa kutoka kwenye hotuba ya Kirigini katika Mkutano wa makamu mwenyekiti John Heche wilayani Tarime ambapo alihoji uimara wa CCM katika Uchaguzi unaochochewa na vyombo vya dola.

"CCM inasema ni chama dume, Ni chama imara kwanini wanatumia vyombo vya dola? mmeona CHADEMA wanaleta vyombo vya dola kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa? Kama wasingetumia vyombo vya dola kubaka ule uchaguzi hali ingekuwaje?"​
Back
Top Bottom