Abdallah Mohamed Nzunda, anayejulikana zaidi kwa majina ya Mkojani au Mkojani Bin Daruesh (Daruweshi), ni mchekeshaji, mwigizaji na mtayarishaji wa maudhui kutoka Tanzania anayejihusisha zaidi na sketi za vichekesho na maonyesho ya kuchekesha.
Anajulikana sana katika tasnia ya burudani nchini kwa kuigiza wahusika wanaogusa maisha ya kila siku ya watu, jambo lililompa umaarufu mkubwa hasa kupitia mitandao ya kijamii. Mara nyingi hutajwa kama msanii nguli wa vichekesho.
Mbali na sanaa, Mkojani aliwahi kuonyesha nia ya kuingia kwenye siasa baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Temeke, Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Hata hivyo hakuteuliwa kuwa mgombea wa chama hicho katika kura za maoni, ambapo taarifa mbalimbali ziliripoti kuwa aliachwa nje ya mchakato huo kumwaga machozi baada ya matokeo ya kura za maoni kutangazwa.
Wakuu!
:D:D sasa hii ndio kazi yako Mkojani, endelea kuchekesha Watu tu!
Mwigizaji na mchekeshaji Abdallah Mohamed Nzunda, maarufu kama Mkojani, amemwaga machozi akidai kufadhaishwa na matokeo ya kura za maoni za Ubunge Jimbo la Temeke kupitia CCM. Adai Wajumbe walimtia moyo sana kuwa atatoboa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.