Abiria (kutoka neno la Kiarabu عبر ˁabara kwa maana ya kuabiri, kuvuka eneo la maji) ni watu wanaosafiri kwa kupanda meli, ndege, gari, basi, pikipiki au treni.
Abiria hutumia vyombo hivyo vya usafiri kama njia ni mbali, au kama hawana usafiri wa binafsi au kama wanapendelea matumizi ya usafiri wa umma kuliko usafiri wao binafsi.
Kwa kawaida wakipanda wanalipia kiasi fulani kama nauli ili mwenye chombo hicho aweze kuwalipa dereva na wahudumu wengine pamoja na gharama za chombo chenyewe na matumizi yake.
Jeshi la Polisi limetoa maagizo kwa makamanda wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanafanya doria katika barabara zote zitakazotumiwa na mabasi yatakayokuwa yanafanya safari zake saa 24 katika kudhibiti aina zozote za kihalifu.
Huo ni utekelezaji wa agizo lilotolewa, Juni 28, mwaka huu na Waziri...
Je wajua vyanzo vya AJALI barabarani? Abiria kuwa kimya bila kukemea au kutoa taarifa polisi dhidi ya makosa yafuatayo:
1: Dereva kuyapita magari ya mbele bila TAHADHARI.
2: Dereva kuendesha gari akiwa amelewa pombe au dawa za kulevya.
3: Dereva kuendesha chombo kwa mwendokasi.
4: Dereva...
Kituo cha mwendokasi Kimara pia usimamizi ni mbovu sana, yaani unakuta magari yapo ya kutosha, abiria wanajaa kituoni kwa zaidi ya saa mbili.
Madereva wanapitapita tu kama hawaoni kinachoendelea,kuna muda magari yanaondoka yakiwa tupu kituoni, yanaacha abiria.
Vituo vya DART Mwendokasi...
Kuna mambo mawili binafsi yananikera katika usafiri wa mabasi ya ruti ndefu tz.
1. Mabishano ya wanaoitwa wanazi wa makampuni ya mabasi juu ya ubora wa gari zinazotumika na kipimo ni mwendokasi.
2. Betting ya basi lipi litawahi kufika eneo Fulani.
Yote haya yanachochea mwendokasi na rafu...
Zamani kabla mifumo ya fedha kuimarika watu wakikuwa wakisafiri na mamilioni ya pesa wakija Dar kununua chochote au kuuza chochote
Sasa hivi watu husafiri tu na hela ya kula njiani tu pesa zote huwa kwenye akaunti
Hivyo tishio la kuwa abiria watavamiwa na kuporwa dogo mno. Hata mporaji hawezi...
Ndege kubwa ya C919 hivi karibuni iliruka kutoka Shanghai hadi Beijing ikiwa na abiria, ikiashiria kuwa ndege hiyo kubwa ya abiria iliyotengenezwa China kwa kujitegemea imeingia katika katika soko la safari za anga.
Utengenezaji wa ndege kubwa unajulikana kama kilele cha kiwango cha viwanda...
Habari wakuu,
Mtindo huu wa bajaji kupakia abiria wawili mbele si mpya, naamini watu wengi mmekutana nayo hii hasa kwa wakazi wa Mbezi ya Kimara. Hili ni jambo hatari ambalo linaweza kusababisha majanga muda wowote, hasa ukizingatia madereva wengi wa bajaji walivyo rafu barabarani.
Kubwa zaidi...
Kuna Mmoja kapanda Dala Dala nililopanda Jana Usiku la Buguruni - Mwenge aliniachi Maswali mengi sana.
Kwanza ana Afya nzuri ambayo hata GENTAMYCINE ninayeombwa Msaada sina.
Pili kuna muda akasema kuwa tayari ana Shilingi Milioni Saba na anataka tumchangie Shilingi Mia Tano, Elfu Moja zetu na...
Rais wa Marekani, Joe Biden ameagiza Wizara ya Uchukuzi kuandika kanuni mpya zitakazoyalazimu Mashirika yote kugharamia Chakula na Malazi ikiwa uchelewaji utakuwa ndani ya udhibiti wa Shirika.
Baadhi ya sababu zitakazochangia kulipwa fidia ni pamoja na Matatizo ya Kiufundi na Shirika...
Salaam Wandugu,
Nimepata taarifa mtandaoni kuwa ndege ya Malaysia iliyopotea miaka tisa iliyopita imekutwa kwenye maji ikiwa haina abiria.
Habari hiyo ilichapishwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Twitter linaonesha picha ya mbele ya ndege yenye kutu inayosomeka: “Ndege ya...
Boti hiyo iliyokuwa imebeba wahamiaji wakielekea Barani Ulaya imezama katika Pwani ya Libya ilikuwa na abiria 60.
Watu watano wamesalimika akiwemo mtoto raia wa Syria, huku Wanausalama wakiwa na kazi ya kuopoa miwili kutoka kwenye bahari.
Libya imekuwa ikitumika kama njia kuvuka kwenda Ulaya...
Kituo cha daladala Kawe ni kero kubwa sana kwa watumiaji wa kituo hicho, Kituo hakina ukarabati wowote, iwe masika na kiangazi, hakuna nafuu, ikiwa kiangazi kituo kinapambwa kwa mashimo na mabonde hali inayoathiri magari na abiria pale wanapofika kituoni.
Kwa masika kama kipindi hiki ndio balaa...
Kituo kikubwa cha daladala kilichopo Kilombero karibu kabisa na Soko la Kilombero jijini hapa kimegeuka kuwa kero kubwa hasa kipindi hiki cha mvua kutokana na kukosekana kwa sehemu ya kujikinga mvua kwa abiria wanaotumia kituo hicho.
Muundo wa kituo hiki umejengwa kama uwanja wa mpira na sio...
Shirika la Ndege Tanzania ATCL ni moja ya mashirika ambayo kwa kipindi cha nyuma walikua na nidhamu ya muda wa kusafirisha abiria kuliko wengine Hususan kipindi cha mwendazake JPM Magufuli, Usiku wa kuamkia jana Aprili 16 nilipaswa kusafiri kutoka Mwanza kwenda Dar majira ya saa 8:30 usiku...
Siku chache baada ya kutokea ajali iliyoua watu 13 mkoani Ruvuma, Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani, Mossi Ndozero amefanya msako ili kubaini malori yanayopakia abiria na mizigo kwa ajili ya kuwasafirisha kwenda minadani.
Ndozero amepiga marufuku usafiri huo kupakia abiria huku akishusha...
Ni wazi kwamba ndege ya ATCL inayokwenda Chato huwa inaenda tupu, bila abiria
Abiria pekee ni mama Janeth Magufuli na watoto wake au Kalemani.
Nashauri ruti hii ifutwe kwa maslahi ya taifa.
Ajali za barabarani zinaepukika ukiachilia mbali matatizo ya kibinadamu. Kuna sababu nyingi sana zimekuwa zikitajwa, lakini mimi niseme mbali na sababu zote hizo zinazotajwa chanzo kikubwa ni abiria wenyewe.
Sijui ni ukosefu wa elimu ya kwa Watanzania au kudharau au kuona muda wote Mungu yupo...
Zikiwa zimepita siku mbili tangu tangu Manispaa ya Ubungo, ianze utaratibu mpya wa kuingia na kadi katika stendi ya mabasi ya Magufuli, mfumo huo umelalamikiwa kuchelewesha abiria, huku baadhi ya madereva nao wakilalamikia ucheleweshaji wa safari zao.
Hatua ya matumizi ya N- Card yalianza...
Manispaa ya Ubungo, imeanzisha utaratibu mpya wa kuingia na kadi katika stendi ya kimataifa ya mabasi ya Magufuli ili kudhibiti upotevu wa mapato kwa abiria wanaoingia katika kituo hicho kilichopo Mbezi Luis.
Hatua ya matumizi ya N- Card iliyoanza leo Jumatatu Februari 20, 2023 imelenga pia...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.