ahukumiwa

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. JanguKamaJangu

    Katavi: Muongoza watalii ahukumiwa miaka mitatu jela kwa kuomba rushwa

    TAKUKURU mkoa wa Katavi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa, Agosti 24, 2022 imefungua shauri la jinai Na. CC. 95/2022 dhidi ya Elisha Christopher Mashamba ambaye ni muongoza watalii katika hifadhi ya misitu ya Tongwe East - Nkondwe Waterfalls Camp. Ameshitakiwa kwa makosa ya kuomba na...
  2. JanguKamaJangu

    Kinyozi atupwa jela miaka 30 kwa kumpa mimba mwanafunzi

    Mahakama ya Wilaya ya Iringa, imemhukumu kinyozi, Batista Ngwale (27) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kumpa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18. Binti huyo alikuwa akisoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kibena iliyopo Iringa Vijijini. Binti aliiambia...
  3. Lady Whistledown

    Mhasibu wa Zamani wa Wizara ya Mambo ya Ndani ahukumiwa kwa Ubadhirifu

    Mhasibu wa zamani Wizara ya Mambo ya Ndani Christina Kaale, amehukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni nane ama kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka manne yaliyokuwa yakiwakabili likiwemo la ubadhirifu wa sh milioni 15.2. Hukumu hiyo imesomwa...
  4. K

    Sudan: Kondoo ahukumiwa miaka mitatu gerezani kwa kuua mtu

    Kondoo mmoja Nchini Sudan ya Kusini amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia na kumuua mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 45. Mmiliki wa kondoo huyo ameamriwa kulipa ng'ombe watano kwa familia ya mwanamke huyo na pia kondoo huyo atatolewa...
  5. Lady Whistledown

    Muigizaji Nchini Nigeria ahukumiwa Miaka 16 jela kwa kumnyanyasa mtoto kingono

    Muigizaji wa Nigeria, Olanrewaju Ominyika (49), maarufu kama ‘Baba Ijesha’ amepatikana na hatia ya kumnyanyasa kingono mtoto wa miaka 14 kati ya mwaka 2013 na 2014 Mnamo Mwaka jana, Omiyinka alikiri mahakamani kumlawiti mwathiriwa, lakini akasema ni katika muktadha wa nafasi aliyokuwa akiigiza...
  6. Lady Whistledown

    Rwanda: Afisa wa Zamani ahukumiwa miaka 20 jela kwa kuhusika katika Mauji ya Halaiki

    Laurent Bucyibaruta, aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Gikongoro Kusini amekutwa na hatia nchini Ufaransa kwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994, ambapo takriban Watutsi 800,000 na Wahutu ambao hawakufungamana na upande wowote waliuawa. Gavana huyo wa zamani anadaiwa kutumia ushawishi wa...
  7. F

    Katibu mkuu CWT taifa ahukumiwa

    Katibu mkuu wa Chama Cha walimu Tanzania CWT amekutwa na hatia hivyo kuhukumiwa yeye na mwenzake muweka hazina kifungo Cha miezi sita Kisha kurejesha fedha hizo baada ya kifungo. Ndugu zangu tusitumie vibaya fedha za walimu tunapopewa nafasi.
  8. mwanamwana

    Mwanamke aliyeandika insha juu ya jinsi ya kumuua mume ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumuua mumewe

    Mwandishi wa kitabu chenye jina lisemalo 'Jinsi ya kumuua mume wako' kutoka nchini Marekani aitwaye Nancy Crampton Brophy, mwenye umri wa miaka 71 amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya mume wake aliyoyatekeleza mwaka 2018. Imeelezwa kwamba tukio la mauaji...
  9. JanguKamaJangu

    Kijana wa miaka 24 jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 9

    Juwai Magoda, mwenye umri wa miaka 24 Mkoani Iringa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na faini ya Tsh milioni moja baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji kwa binti wa miaka 9 aliyekuwa akisoma darasa la pili. Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Wilaya ya Iringa, inadaiwa Magoda...
  10. GENTAMYCINE

    Ahukumiwa kwa Kupiga Punyeto mara tatu mfululuzo ndani ya Ndege ikiwa angani inakata Mawingu mazito

    Abiria wa shirika la ndege la Southwest Airlines aliyeshutumiwa kwa kupiga punyeto mara kadhaa wakati wa safari ya ndege kutoka Seattle kwenda Phoenix mwezi uliopita amehukumiwa kifungo cha siku 48 gerezani, waendesha mashtaka wa serikali wamesema. Antonio Sherrodd McGarity, (34) mkazi wa...
  11. Lady Whistledown

    Misri: Mmiliki wa vyombo vya habari ahukumiwa kwenda jela miaka 3 kwa kuwanyanyasa kingono watoto yatima

    Mahakama nchini Misri imemhukumu tajiri wa vyombo vya habari kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuhusika katika biashara haramu ya binadamu na kuwanyanyasa kingono mabinti wenye umri mdogo katika kituo cha watoto yatima alichoanzisha. - Mohamed al-Amin ambaye ni mmiliki wa Future Media, CBC...
  12. JanguKamaJangu

    Mwanariadha wa Ujerumani ahukumiwa kifungo miezi 6 kwa SMS za vitisho kwa Wanawake waliowatongoza wakamkataa

    Mwanariadha wa Ujerumani amehukumiwa kifungo cha Jela miezi sita au kulipa faini ya Ksh. 70,000 (Tsh. Milioni 1.3) kutokana na kosa la vitisho na udhalilishaji wa mtandaoni Nchini Kenya. Weiss Marvin Valentin, 25, alitenda kosa hilo mwaka 2022 kwa kutoa matamshi ya kukera na kutishia kusambaza...
  13. beth

    Rwanda: Mchina aliyerekodiwa akimpiga mfanyakazi aliyefungwa kwenye mti ahukumiwa kifungo cha miaka 20

    Mahakama Nchini humo imemhukumu Mfanyabiashara ambaye ni Raia wa China kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kurekodiwa akimpiga Mwananchi mwaka 2021 Sun Shujun alikuwa anakabiliwa ya Mashtaka ya kupiga Wafanyakazi wake waliokuwa wanatuhimiwa kwa wizi, ambapo katika video iliyorekodiwa...
  14. Chachu Ombara

    Kigoma: Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua jirani yake

    Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mtu mmoja aitwaye Kinyota Kabwe mkazi wa Muzye wilayani Kasulu kwa kosa la kumuua kwa makusudi jirani yake kwa kumchoma mkuki mara tatu na kusingizia alikuwa amechanganyikiwa. Kesi hiyo namba 105 ya Jamhuri dhidi ya...
  15. John Haramba

    Dereva lori la mafuta ahukumiwa jela miaka minne na faini milioni 16

    Mahakama ya Mkazi Wilaya ya Iringa imemfunga jela miaka minne pamoja na kulipa fidia ya shilingi 16,050,000 dereva wa lori la mafuta la Kampuni ya Panone And Co. Ltd, Faid Mussa Manis baada ya kupatikana na hatia katika kesi jinai namba 2019 iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake 6...
  16. Analogia Malenga

    Njombe: Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumbaka mara mbili Mwanafunzi

    Furaha Samweli Ligate (26) mkazi wa kijiji cha Unyangala wilaya ya Makete mkoani Njombe amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mara mbili mtoto mwenye umri wa miaka 15 aliyekuwa amehitimu darasa la 7 mwaka 2021 akisubiri kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wa 2022 Hukumu...
  17. Roving Journalist

    Lindi: Selemani Matola (53), ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumnajisi Mjukuu wake

    Mahakama ya hakimu mkazi wilaya Lindi imemuhukumu Selemani Matola (53) mkazi wa Halmashauri ya Mtama kifungo cha maisha gerezani baada ya kukutwa na hatia ya Kumnajisi mjukuu wake mwenye umri wa miaka 8 Inadaiwa kuwa mshatakiwa huyo alifanya tukio hilo Disemba 17,2021 usiku wakati mkwewe...
  18. beth

    Myanmar: Aung San Suu Kyi ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela

    Kiongozi wa Myanmar aliyetolewa Madarakani na Jeshi amehukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani, ikiwa ni mwanzo wa kutolewa hukumu ambazo zinaweza kupelekea afungwe jela maisha Aung San Suu Kyi ambaye amekuwa kifungo cha nyumbani tangu Februari 2021 baada ya Jeshi kufanya Mapinduzi...
  19. Suley2019

    Korea Kaskazini: Ahukumiwa kunyongwa kwa kutazama na kusambaza nakala za series ya 'Squid Game'

    Mwanaume mmoja raia wa Korea Kaskazini ambae utambulisho wake haujawekwa wazi amehukumiwa kifo kwa kutazama na kusambaza nakala za series maarufu kutoka Netflix 'Squid Game'. Inasemekana hukumu ya kunyongwa kwake hadi kufa ia tatekelezwa na kikosi maalumu cha kurusha risasi. Mbali mwanaume...
  20. tang'ana

    Serengeti: Ahukumiwa miaka mitatu jela kwa wizi wa mbuzi

    Mkazi wa kijiji cha Nyiboko, kata ya Kisaka, Mwita Karege (19) amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri kuiba mbuzi watatu wenye thamani ya Sh150,000. Hukumu hiyo katika kesi ya Jinai namba 326/2020 imesomwa leo Jumatatu Oktoba 25 na hakimu...
Back
Top Bottom