Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ameliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani humo kumsaka na kumtia nguvuni, Andrea Ngomeni, mkazi wa Kijiji cha Kambikatoto wilayani Chunya kwa tuhuma za kuuza eneo la pori la akiba la hifadhi ya msitu wa asili...