Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, ameonyesha wasiwasi wake juu ya hali ya demokrasia ndani ya vyama vya siasa nchini, akisisitiza kuwa vyama vingi vimejikita katika kuongozwa na viongozi badala ya kuheshimu matakwa ya wanachama...