buriani

  1. Teknocrat

    TANZIA Nguli wa Soka Duniani, Mbrazili Pele afariki dunia

    Nyota huyo wa zamani wa Santos FC, anayetambuliwa kama mmoja wa Wanasoka bora zaidi wakati wote, alilazwa hospitalini tangu Novemba 29, 2022 huko Sao Paulo Ripoti ya utabibu kabla ya Krismasi ilionyesha alihitaji uangalizi kwa ajili ya ugonjwa wa moyo na figo, na amekuwa akipambana na saratani...
  2. Mohamed Said

    Taazia: Buriani Mja wa Kheri Sheikh Salim bin Ahmed Bajaber

    TAAZIA: MJA WA KHERI SHEIKH SALIM BIN AHMED BAJABER Nimepata taarifa hii leo mchana kuwa Mzee Salim Ahmed Taib Bajaber Mkurugenzi Mkuu wa Pembe Flour Mills (PFM) amefariki Mombasa na kazikwa Markaz Madina, Amkeni Kikambala. Nilimfahamu Mzee Salim mwanzoni mwaka wa 2004 yeye na wakurugenzi...
  3. Mohamed Said

    Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

    BURIANI HASSAN CHIKUSA MSOMI MKIMYA Naamini si wengi wanamfahamu Hassan Chikusa na yote yaliyomsibu katika maisha yake. Mimi nilimjua Hassan Chikusa kwa kuwa alikua jirani yangu akiishi kwa ndugu yake Masaki jirani na nyumba niliyokuwa naishi mimi na familia yangu. Wakati ule alikuwa kijana...
  4. Mohamed Said

    Buriani Sheikh Abdallah Muhsin Barwani

    BURIANI SHEIKH ABDALLAH MUHSIN BARWANI Leo jioni nimepokea taarifa ya kifo cha Shekh Abdallah Muhsin Barwani aliyekuwa akiishi Dubai. Sheikh Abdallah Muhsin ni mdogo wake Sheikh Ali Muhsin Barwani mmoja wa viongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP). Sheikh Abdallah Muhsin amezikwa jana...
  5. Mohamed Said

    Buriani rafiki yangu wa udogoni, Ibrahim Mussa Panzi

    BURIANI RAFIKI YANGU WA UDOGONI IBRAHIM MUSSA PAZI Nimesoma taarifa ya kifo cha Ibrahim Mussa Pazi nikiwa katikati ya Bahari ya Hindi nikitokea Zanzibar kurejea Dar es Salaam. Ibrahim tumekuwa sote udogoni tukicheza mpira Saigon. Huu ni mwaka wa 1966 umri wetu haujapita Miaka 15. Leo...
  6. Mohamed Said

    Buriani Suleiman ''Baku'' Ismail

    BURIANI NDUGU YANGU SULEIMAN ‘’BAKU’’ ISMAIL Siku ya Alkhamis, tarehe 9 tumemzika ndugu yetu Baku mtu maarufu kupita kiasi Mafia. In Shaa Allah nitakuja kueleza umaarufu wa Baku baadae. Ningeweza kuweka picha nyingine yoyote lakini hii picha ya pili niliyoweka hapo chini amejilaza kwenye sofa...
  7. Mohamed Said

    Mazungumzo ya Buriani Oktoba 1968

    MAZUNGUMZO YA BURIANI OCTOBER 1968 Hapo chini Aisha ''Daisy'' Sykes anaeleza mazungumzo ya buriani, mazungumzo ya kuagana kati ya baba yake Abdulwahid Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwa Mwalimu Msasani. Ilikuwa mwezi October 1968 wakati huo Daisy mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha...
  8. Roving Journalist

    Balozi Batilda Buriani: Mtoto aliyeandika Barua ya kuacha Shule, ana akili sana

    "MTOTO ALIYEANDIKA BARUA YA KUACHA SHULE ANA AKILI SANA" RC TABORA "Niliongea na mkuu wa mkoa wa Mtwara baada ya kuona barua ya mtoto aliyetaka kuacha shule, nikamwambia huyu mtoto ana akili sana kwasababu haiwezekani mwanafunzi mtoro aandike barua kama hiyo, nikamwambia mkuu wa mkoa wa Mtwara...
  9. M

    Buriani Mzee Nalaila Lazaro Kiula; Mwadilifu aliyeponzwa na Mfumo kifisadi

    Usiku wa kuamkia Jana amepumzika Mzee Nalaila Lazaro Kiula. Alipata kuwa Mbunge wa Zamani wa Iramba, na Waziri wa zamani wa Ujenzi na Mawasiliano, Naibu wa Waziri wa Elimu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Mzee Kiula ni mojawapo ya Wahanga wa siasa za fitna, majungu na mitandao ndani ya CCM. Akiwa...
  10. M

    Buriani Askofu Mstaafu Amos Luther Gimbi,KKKT Dayosisi ya Kati

    Maisha ya Mwanadamu mwisho wake ni kifo...Bila Shaka mwisho tunaouzungumzia ni hapa Duniani! Lakini kwa Waamini kifo ni mwanzo wa Maisha mapya ya Watakatifu! Mzee Amos Luther Gimbi baada ya Miaka 88 ya Huduma yake hapa Duniani alipumzika tarehe 28.09.2021 huko Marekani! Askofu Dr.Gimbi alikuwa...
  11. Bujibuji Simba Nyamaume

    Buriani Zackaria Hanspope

    Mfanyabiashara mkubwa wa tasnia ya usafirishaji nchi Zacharia Hanspope amefariki usiku huu. Zacharia Hanspope pia alikuwa mdau mkubwa wa michezo, na mpaka mwisho wa uhai wake alikuwa ni mjumbe wa kamati ya ligi.l na mwanachama mahiri wa club ya Simba. Salamu zangu za pole ziende kwa familia ya...
  12. Jemima Mrembo

    TANZIA Buriani Mama Tumaini Kakuyu Mlewa, Mpambanaji hodari, mwasisi wa shughuli za usafi maofisini na upambaji wa kumbi za mikutano, sherehe nk

    Tumaini Kakuyu Mlewa alikuwa ndiye mtu wa Kwanza kuwa na kampuni professional ya usafi akichukua tenda kwenye ofisi za makampuni mbalimbali, mahospitali viwanda nk kupitia kampuni yake ya Fame Consolidated Services LTD. Pia aliasisi shughuli za upambaji wa kumbi za starehe, mikutano etc. Huyu...
  13. Shujaa Mwendazake

    Buriani: Babu wa Loliondo kuzikwa kesho kijijini Samunge

  14. Mohamed Said

    Buriani Rafiki Yangu Waziri ''Maestro" Ally

    BURIANI RAFIKI YANGU WAZIRI ''MAESTRO'' ALLY Hakika sisi ni wa Allah na kwake ni marejeo yetu. Kifo hakizoeleki hata kidogo. Nimepokea taarifa ya kifo cha rafiki yangu Waziri kwa mshtuko mkubwa. Nimejuana na Waziri mwaka wa 1979 wakati huo mimi mwanafunzi Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM)...
  15. X_INTELLIGENCE

    TANZIA Buriani Paul Buchira Katamuzi - (CATAUX Computer. co)

    Nasikitika sana kuwatangazia kifo cha mwanajamiiforums Paul Buchira Katamuzi sijajua kuwa humu alikuwa anatumia jina gani ila alikuwepo na mara nyingi alikuwa anaizungumzia ofisi yake {CATAUX COMPUTER} iliyokuwa inahusika na ufundi kompyuta ama simu na uuzaji wa vifaa vya simu na kompyuta...
  16. Bujibuji Simba Nyamaume

    TANZIA Buriani Peter Richard Mwendamseke

    Peter Richard Mwendamseke alikuwa kijana mjasiriamali, akijikita zaidi kwenye mifumo wa mawasiliano. Pia Peter Richard Mwendamseke alikuwa ni mdau mkubwa wa burudani na michezo. Hakika wana Mbeya wamempoteza kijana wao mahiri. Mungu ailaze Roho ya marehemu mahala pema. Amina
  17. Mohamed Said

    Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu

    Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu! Leo jioni katika makaburi ya Kisutu tumemzika Wendo Mwapachu. Nimemjua Wendo kwa kujulishwa kwake na Ted kama tulivyozoea kumwita. Ted sasa hivi Chief Edward Makwai wa Siha ndiye aliyenijulisha kwake. Wao ni ndugu wa damu na ni siku hiyo hiyo nilimjua...
  18. Deus J. Kahangwa

    Huyu ndiye Padri Privatus Mutekanga Karugendo (1956-2021)

    Hayati Privatus Mutekanga Karugendo: 1956-2021 Tangu mwaka 1990 nilipokuwa kidato cha tatu katika Seminari ya Katoke (Biharamulo) hadi leo nimemfahamu Hayati Privatus Mutekanga Karugendo (65) chini ya kofia tofauti. Nimemfahamu kama mwanateolojia, mwanafalsafa, mchambuzi wa masuala mtambuka...
  19. MTV MBONGO

    Maoni: Dkt. Batilda Buriani ameshushwa mno kuteuliwa kuwa Katibu Tawala

    Dkt. Batilda Buriani alikuwa Balozi Kenya na Japan, Leo kateuliwa kuwa Katibu Tawala mkoa!! Ni kudhalilishwa mno, ni mawazo yangu. Angepewa hata ukuu wa Mkoa.
  20. Mohamed Said

    TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

    BURIANI BABA, RAFIKI NA MZUNGUMZAJI WANGU BALOZI ABBAS KLEIST SYKES Mwezi October 1999 nilikuwa Dubai na nikikaa Carlton Hotel. Siku moja jioni simu yangu ikalia. Walikuwa BBC London Idhaa ya Kiswahili wanataka kunihoji kuhusu Mwalimu Julius Nyerere ambae wakati ule alikuwa amelazwa St...
Back
Top Bottom