chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. Analogia Malenga

    #COVID19 Muungano wa Ulaya kurudisha mamilioni ya chanjo za COVID-19 Afrika

    Muungano wa Ulaya utarudisha mamilioni ya dozi ya chanjo za Johnson & Johnson zilizotengenezwa Afrika Kusini katika bara la Afrika. Mjumbe maalum wa Muungano wa Afrika Strive Masiyiwa amewambia waandishi wa habari kwamba chanjo zote zinazotengenezwa “zitabakia Afrika na kusambazwa Afrika”...
  2. J

    Gwajima, Polepole na Silaa waitwa Kamati ya Maadili ya CCM

    Dodoma. Wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Mbunge wa Kuteuliwa, Humpherey Polepole watawekwa kikaangoni leo na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM kuhojiwa kuhusu masuala tofauti. Wabunge wengine watakaohojiwa leo ni Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga) ambao...
  3. M

    Kwa hali hii naamini maneno ya Askofu Gwajima kuwa viongozi wamehongwa ili chanjo ije

    Huu ni mkusanyiko wa watu ktk Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam mbele ya Rais 02/09/2021. Halafu bila soni akasisitiza chanjo. Hivi Rais Samia yuko serious na gonjwa hili ama anaongea kuwafurahisha na kuwapumbaza walotoa hela? Wenye akili wameamua kumchana mheshimiwa rais bila woga.
  4. Analogia Malenga

    #COVID19 Kassim Majaliwa: Wanaopinga chanjo ni wale ambao hawajaguswa na corona kwenye familia

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wanaopinga chanjo ya #COVID19 hawajaguswa na virusi hivyo katika familia zao, wakiguswa watatafuta chanjo. Amesisitiza chanjo sio lazima lakini ni muhimu. Wataalamu waliotumika kuchunguza chanjo ni wataalamu wa ndani ambao hawawezi kutaka kuwauza watu wao...
  5. beth

    #COVID19 Rais Samia: Silazimishi watu kupata chanjo, kila mtu ni mkubwa ana akili yake

    Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Zinga, Bagamoyo amesema halazimishi watu kupata Chanjo dhidi ya COVID-19 akieleza, "Kila mtu ni mkubwa ana akili yake. Vituo vipo ukijihisi unataka kwenda nenda, ukiona bado hutaki ni wewe na maamuzi yako" Amesisitiza "Tusidanganyane, COVID-19 ipo na inachukua...
  6. stakehigh

    Chanjo ya majaribio ya VVU yashindwa kuleta matokeo chanya barani Afrika

    Chanjo ya VVU ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa shauku sana ya Johnson & Johnson imeshindwa kuonesha uwezo wa kutosha katika jaribio lililohusisha zaidi ya wanawake 2,600 Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ingawa chanjo ilionekana kuwa salama, bila athari mbaya, ufanisi wake katika kuzuia maambukizo ya...
  7. MsemajiUkweli

    #COVID19 Baada ya kampeni ya chanjo za COVID-19 kudoda, Askofu Gwajima kuwa mbuzi wa kafara?

    Kinachoendelea serikalini na bungeni ni kutafuta mbuzi wa kafara baada ya “utapeli” wa serikali kuhusu chanjo za korona kushtukiwa na wananchi wengi nchini. Fikiria chanjo za watu milioni moja ambazo serikali ilipokea kama “msaada” kutoka Marekani mpaka sasa zaidi ya nusu yake bado ziko kwenye...
  8. O

    #COVID19 Baada ya Idadi, tunahitaji kujua na muda wa Matumizi ya Chanjo

    Tangu tarehe 4 hadi sasa Waliopokea Chanjo ya Uviko ni wananchi wapatao laki 3 na kadhaa sawa na 30% ya chanjo tulizopokea, ambayo ni sawa na mwezi mmoja tangu kuanza kutolewa, Kama Serikali itaendelea na Kasi hii itachukua miezi 3 na kadhaa kuzimaliza hizi chanjo. Hoja yangu kwa serikali, Kama...
  9. BestOfMyKind

    Ng'ombe 25 wafa baada ya kupata chanjo dhidi ya homa ya mapafu

    Dar es Salaam. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameagiza kusakwa na kukamatwa kwa wataalamu wa mifugo, waliotoa chanjo ya homa ya mapafu kwa mifugo katika Kijiji cha Mlazo, wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Taarifa iliyotolewa leo Jumatano, Septemba Mosi 2021 na Wizara ya Mifugo na...
  10. Analogia Malenga

    Spika Ndugai: Gwajima akirudia tutamuita Waziri wa Mambo ya Ndani na kumhoji

    Spika Job Ndugai amesema vyombo vingine vya serikali na chama vinapaswa kumuwajibisha Josephat Gwajima kutokana na kauli zake Amesema kama hatowajibiswa na akarudia makosa aliyokutwa nayo kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge watalazimika kuitwa wao Amesema Waziri wa Mambo ya Ndani atapaswa...
  11. kagoshima

    #COVID19 Wapinga chanjo (Gwajima et al) wana macho lakini hawaoni

    Inawezekana ugumu wa kuelewa hurithiwa. Coverage ya chanjo ya gonjwa la Covid Uingereza ni zaidi ya 70% . Angalia viwanjani kwenye premiere league England ni full. Watu hawavai barakoa tena viwanjani. Njoo huku bongoland unawakuta much know just for political gain, wahamasishaji kuzuia watu...
  12. Francis fares Maro

    Chanjo ni hiari lakini ina umuhimu

    Tokea nimezaliwa na sio Mimi tu, watanzania wengi kama sio wote tumekua tunapata chanjo kutoka Kwa wahisani (mabeberu)..kila chanjo lazima iwe na side effects Kwa baadhi ya watu lakini sio wote. hanjo hizi zina umuhimu mkubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku!!..tuache propoganda mbaya za...
  13. N

    Askofu Gwajima ashindwa kutoa ushahidi wa tuhuma zake dhidi ya chanjo

    Katika kikao kinachoendelea Bungeni leo agosti 31, Kamati ya maadili iliyowahoji Askofu Josephat Gwajima na mbunge Jerry Slaa imetoa ripoti yake na mapendekezo ya adhabu. Kwa upande wa askofu josephat Gwajima, Kamati imesema kua ilimtaka atoe evidence juu ya zile tuhuma alizokua...
  14. Analogia Malenga

    #COVID19 Zanzibar: Waliochoma Sinovac watakiwa kupata J&J ili kwenda Hijja

    Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema wanaotaka kwenda Hijja ambao wamechoma chanjo ya Sinovac wanatakiwa kuchoma tena chanjo ya Johnson & Johnson kwa sababu Saudia haiitambui chanjo ya Sinovac Sinovac ilianza kutolewa Zanzibar July 23, 2021 kwa kuwa ilikuwa imepitishwa na...
  15. Jasusi Mbobezi

    #COVID19 Chanjo milioni moja hazijaisha tu?

    Siku moja nilimsikia mheshimiwa sana waziri wangu wa Afya akisema watu wanajitokeza kwa wingi kudungwa kuliko walivyo tarajia, siku nyingine nikamsikia mheshimiwa sana Rais Samia Suluhu akisema kuwa kinacho muumiza kichwa kwasasa ni wapi watapata chanjo zaidi, maana kwa jinsi hizi za awali...
  16. Sam Gidori

    #COVID19 Wanasayansi wanatengeneza Chanjo ya Corona inayoweza kuliwa kwenye Nyanya

    Wanasayansi nchini Uzbekistan wanatengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona inayoweza kuliwa ndani ya nyanya, Wizara ya Ubunifu ya nchi hiyo imeeleza. Wanasayansi kutoka Chuo cha Sayansi wamefanikiwa kuweka sehemu ya kirusi hicho ndani ya seli ya nyanya ambapo seli hiyo imegeuka kuwa chanjo...
  17. Analogia Malenga

    Msemaji Mkuu wa Serikali: Zaidi ya watu 300,000 wapata chanjo

    Zaidi ya Watanzania 300,000 wamepatiwa chanjo ya UVIKO -19 huku mikoa ya Kanda ya kaskazini ikiongoza kwa idadi ya watu wengi. Idadi hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 31 ya dozi zililoletwa awamu ya kwanza mwezi Julai ambazo zilikuwa 1,058,400 zilizosambazwa katika vituo 550 nchini kote...
  18. Z

    #COVID19 Kumbe askofu Gwajima aweza kuwa sahihi: Tangia chanjo ya COVID-19 inatolewa mpaka tarehe 23 Agosti ilikuwa partially approved kutolewa kwa binadamu

    Swali ni je imekuwa scientifically approved au politically approved? The F.D.A. approved full licensure of the Pfizer vaccine this morning and has also, I’m sure you’re aware, back in August on the 9th, the secretary articulated that it was his intent to mandate Covid-19 vaccines upon F.D.A...
  19. Poppy Hatonn

    #COVID19 Leo nimekwenda Muhimbili kuchanja Corona halafu nimeogopa, nimerudi

    Leo, yaani jana Jumamosi nimekwenda Muhimbili kuchanja Corona. Nimeingia katika geti, nilikuwa nashangaa shangaa pale akaja mwanamke mmoja akaniuliza, "Kwani ulikuwa unataka kwenda wapi?" Nikamwambia nataka kuchanja Corona. Akaniambia pita pale hospitali ya Jakaya, halafu mbele kule kuna jengo...
  20. M

    Gwajima alifuata ushauri wangu kukataa kujibu maswali ya kamati ya bunge. Bunge halina mamlaka hayo

    Siku moja kabla Askofu Gwajoma hajahojiwa na kamati ya bunge niliibua uzi unaosema bunge halina mamlaka ya kumuhoji alichoongea kanisani. Hivyo nikashauri Gwajima akatae kujibu swali lolote atakaloulizwa. Nilisema wazi ninampinga Gwajima msimamo wake wa kutotaka watu wachanjwe kwani mimi...
Back
Top Bottom