chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. B

    Mahasimu wa CHADEMA, Mbowe na Chanjo tukutane hapa

    Baada ya kuchukua muda kufuatilia maoni na mitizamo ya wajumbe mbalimbali kiroho safi, nimejiridhisha pasi na shaka yoyote kuwa: "Pana wajumbe wenye kujawa na hasira kali isiyokuwa na maelekezo kuhusiana na Mh. Mbowe, Chadema, Chanjo za Corona na tahadhari zake." Wajumbe hao wakisikia moja...
  2. Analogia Malenga

    #COVID19 Ndugai: Chanjo ni hiyari ila hauna hiyari kuambukiza wenzako

    Wakati kukiwa na mjadala wa baadhi ya wabunge kuhusu chanjo ya corona inayoendelea kutolewa nchini, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema pamoja na chanjo kuwa hiari, haimfanyi mtu kuwa na hiari ya kuambukiza wengine. Kauli hiyo imekuja kukiwa tayari kuna wabunge walioonyesha wazi kupingana na...
  3. JU60_tz

    #COVID19 Chanjo ya Corona imetengenezwa kwa vitu gani?

    Je, vitu hivyo ni siri? ni kwanini viwe siri wakati haya ni mapambano ya Dunia nzima na tunasema kuwa tunashirikiana kupambana na janga hili!? Je, wataalamu wetu wa Afya Tanzania wanavifahamu vitu hivyo? kama ndiyo kwanini wasimwambie MAMA ili tuvipate tuweze kutengeneza chanjo yetu wenyewe...
  4. Mtemi mpambalioto

    #COVID19 Ushauri kwa Serikali: Kupima COVID-19 iwe bure baada ya hapo ndio mtu akachome chanjo

    Huu ni ushauri mkubwa kwa serikali: Kitaalamu chanjo inatakiwa uchanjwe kama hauna vimelea vya ugonjwa husika. Sasa iweje watu wanaenda wanachoma chanjo tu bila kujua status zao? Je, Serikali hamuoni kuwa hili ni tatizo? Hata vifo vinavyotokea kwa walichoma chanjo vinachangiwa na tatizo hili...
  5. beth

    #COVID19 Marekani: CDC yapendekeza wajawazito kupata chanjo ya Covid-19

    Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kimesema Wanawake Wajawazito wanaweza kupata Chanjo dhidi ya COVID19 ikisema hakuna hofu yoyote ya usalama wao katika Uchambuzi mpya uliofanyika. CDC imesema inatambua kauli kuhusu uzazi ambazo zimekuwa zikisambaa, lakini maneno hayo hayana ushahidi...
  6. T

    #COVID19 FDA ya Marekani yaidhinisha dozi ya tatu ya chanjo ama booster vaccine kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19

    Taasisi ya Chakula na Dawa ama FDA ambayo ndio huithinisha matumizi ya madawa kwa binadamu nchini Marekani inatarajia kuidhinisha matumizi ya dozi ya pili ya chanjo ama booster vaccine shots (kwa waliopata Chanjo ya Johnson and Johnson) ama ya tatu kwa waliopata chanjo nyingine kama Moderna ama...
  7. Analogia Malenga

    #COVID19 Zaidi ya watu 9,000 wamepata chanjo, hakuna madhara yaliyoripotiwa

    Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema hakuna madhara yaliyoripotiwa kutokana na chanjo za #COVID19. Tangu kuanza kwa zoezi la utoaji chanjo zaidi ya watu 9,000 wamepatiwa chanjo hadi sasa. Zoezi la utoaji chanjo linaendelea bara na visiwani kwa hiyari.
  8. N

    #COVID19 Kwa anayejua tunapataje kadi za chanjo ya COVID-19 tujuzane

    Tuna zaidi ya wiki sasa tangu tuchanjwe chanjo ya COVID19 kwa mbwembwe sana huku makao makuu ya nchi lakini mpaka sasa hakuna taarifa ya uhakika juu ya lini na kwa njia gani tutapata hizo kadi za chanjo. Nikiuliza pale Benjamini Mkapa Hosp naambiwa mara tunasubiri za online mara tunasubiri...
  9. S

    Changamoto juu ya chanjo iliyotokea miaka ya 1950s ndio inayojitokeza sasa, ila mwishoni utafika tu

    Nianze kwa kusema kuwa wenzetu ambao ni jirani zetu hapo kenya nao walianza kwa kusema kuwa chanjo ya Corona ni hiyari na sio lazima , lakini tamko lilitoka jana kutoka serikalini ni kwamba kila Mkenya ambaye ni mtumishi wa Umma lazima apate chanjo ndani ya wiki mbili zijazo na mwisho ni tarehe...
  10. beth

    #COVID19 Guinea: Watumishi wa Umma watakiwa kuwa cheti cha kupata chanjo ya COVID-19

    Watumishi wote wa Umma Nchini humo watatakiwa kuonesha ushahidi kuwa wamepata chanjo dhidi ya COVID19 kabla ya kuruhusiwa katika maeneo yao ya kazi Rais Alpha Condé ametoa maelekezo kwa Waziri Mkuu kuhakikisha Mawaziri wote pamoja na Watumishi wengine Serikalini wanapata Cheti ili kuruhusiwa...
  11. B

    #COVID19 Kenya: Chanjo ya Covid lazima kwa watumishi wa Umma

    Kuwa na dhamana ya maisha ya watu ni pamoja na kuwajibika zaidi hata dhidi ya ujinga wao. Babu wa Loliondo angekuwa hai Kenya lakini si Tanzania. Heko rais Kenyatta kwa maana heri lawama kuliko fedheha. Kenya kwa mtumishi wa umma, chanjo ni lazima. Pole pole tutafika tu. Kwanza Janssen...
  12. Makirita Amani

    #COVID19 Hii hapa ni nafasi yako ya kuibadili dunia, itumie

    Rafiki yangu mpendwa, Kama umewahi kudhani kwamba huwezi kuibadili dunia umekuwa unakosea sana. Kila mmoja wetu kuna kitu anaweza kufanya kuibadili dunia na kuifanya kuwa sehemu bora kabisa ya kuishi. Na leo hapa unakwenda kujifunza kitu kimoja unachoweza kufanya hapo ulipo na ukaibadili sana...
  13. MR TOXIC

    #COVID19 Hoja za Askofu Gwajima zimewaumbua wataalam wetu na waliomuingiza 'mkenge' Rais Samia kwenye chanjo ya Corona

    Nilitegemea wataalam wetu wa afya pamoja na washauri wa Rais waliomshauri kuagiza chanjo ya corona watakuwa mstari wa mbele kujibu hoja za askofu badala yake wamekuwa watu wa kumshambulia yeye binafsi na kumpa vitisho badala ya kujibu hoza zake kitaalam. Katika hoja ya kwanza, Askofu gwajima...
  14. Analogia Malenga

    #COVID19 DC wa Busega azindua utoaji chanjo

    Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria amezindua rasmi zoezi la chanjo ya UVIKO 19 (COVID 19) Wilayani Busega, uzinduzi uliofanyika Hospitali ya Wilaya ya Busega, huku akiwataka wananchi kupuuza maneno na taarifa za kizushi zinazoendelea kusambaa kwenye baadhi ya Mitandao kuhusu chanjo...
  15. GUSSIE

    #COVID19 If you cannot question it, it's not science, It's propaganda

    Mimi nimechanjwa chanjo ya P fizer muda mrefu wakati hapa kwetu tukihubiri malimao na matangawizi, Tuliimba pambio wote za ujasiri wakati huo kuwa beberu hafai na chanjo hazifai Leo bila aibu na Haya wana CCM tumegeuka ghafla na kuanza kudance ngoma ya mwenyekiti wa chama Nimeandika uzi huu...
  16. M

    #COVID19 Mambo niliyoyaona baada ya kupata chanjo leo

    Leo nimechanjwa katika mji mmojawapo wa wilaya. Nilifanya booking online na tarehe yangu niliyochagua ilikuwa jana bahati mbaya jana hawakufungua. Nilichokiona ni: Pamoja na kueleza kuwa nilikuwa na booking online lakini hiyo haikuwa na uzito ila nilipewa fomu ya kujaza. Mtumishi alikuwa mmoja...
  17. N

    #COVID19 Sijui kama mtazamo wangu uko sawa, ila nawaona wote wanaopinga chanjo kama wana shortage kichwani!

    Mweshmiwa mbunge wa viti maalumu Humphrey Polepole yeye anasema tusipige chanjo ila tufanye mazoezi kwa wingi pia tule ugali wa dona na matembele kwa wingi na kuondoa hofu tutaishinda corona Askofu yeye anadai tumuomne sana Mungu kwani alikua ameshaliponya taifa na korona ikaisha, pia analaumu...
  18. J

    #COVID19 Tundu Lissu: Leo nimekamilisha chanjo ya Corona kwa kuchomwa sindano ya pili, mimi nimechanja Astra Zeneca!

    Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amewataka Watanzania wote kujitokeza na kuchanja ili kwa pamoja tuishinde na kuitokomeza Corona. Lissu amesema leo hii 09/08/2021 amekamilisha chanjo yake ya Corona kwa kuchoma sindano ya pili na kwamba yeye amechanja aina ya Astra Zeneka. Mungu ni...
  19. Analogia Malenga

    #COVID19 UN: Taarifa feki kuhusu chanjo zinazidisha muda ambao ungetumika kudhibiti maambukizi

    Umoja wa Mataifa(UN) umesema taarifa zisizo sahihi kuhusu chanjo ya #COVID19 kunarefusha muda ambao ungetumika kudhibiti maambukizi ya Corona. UN wametoa wito kwa raia kuhakiki taarifa kabla ya kusambaza taarifa hizo kwa wengine ambazo zinaathiri mapambano dhidi ya Corona. Wamesema taarifa za...
  20. Analogia Malenga

    #COVID19 Iran: Rais apata chanjo iliyotengenezwa na Wairan wenyewe

    Rais wa Iran Ebrahim Raisi ambaye ameapishwa hivi karibuni, amepata chanjo ya #COVID19 ya COVIran Barekat. COVIran ni moja ya chanjo inayotengenezwa Iran ambayo ipo katika mchakato wa kuidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Maambukizi ya COVID19 yameongezeka na vifo zaidi ya 500...
Back
Top Bottom