chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. H

    #COVID19 Wataalam wa Afrika Kusini waukubali Ubora wa Chanjo ya Johnson & Johnson

    Sote tunafahamu kuwa Afrika Kusini ndiyo nchi inayoongoza katika bara la Afrika katika huduma bora za afya na teknolojia ya afya. Afrika Kusini, kwa takwimu rasmi, ndiyo inayoongoza katika maambukizi na vifo vinavyotokana na covid 19, japo kiuhalisia hatujui kama huo ndio ukweli wenyewe au ni...
  2. #COVID19 Askofu Gwajima: Nasubiri wataalamu wa ndani wa chanjo ya COVID-19 waongee kisha nitawapiga kwa risasi moja tu watawanyike

    Gwajima anasema viongozi na wataalamu wetu ni vigeugeu na hawafai kuongoza, Wanafanya mambo kwa kuangalia upepo na sio utaalamu Anasisitiza wajiuzulu mapema kwenye suala la covid-19 Akihutubia maelfu ya waumini wake leo Gwajima amesema wataalamu wetu ndio hao walijenga pale Muhimbili jiko la...
  3. #COVID19 Waoga wa Sindano: Mikakati gani tutumie kuchanjwa?

    Niseme tu mimi binafsi sina tatizo lolote na chanjo. Yaani kama ingekua sio huu uoga uliopitiliza wa sindano, mimi ningekua kati ya watu wa mwanzo kabisa kuchanjwa! Lakini mpaka leo bado nambwelambwela kwenda kuchanjwa kisa tu naogopa ile sindano. Kama mliona ile video ya mwanajeshi aliepelekwa...
  4. E

    Ogopeni ugonjwa msiogope chanjo

    Eti baada ya kuogopa gonjwa la Corona wanaogopa chanjo yake pumbafu. ukipata ugonjwa kuupona unatumia hela nyingi mpaka unafirisika na pengine usipone, kuna jirani yangu kamtibu mkewe kwa gharama ya sh 29 million bahati nzuri amepona lakini mume huyo hoi kiuchumi. Kamwa wewe ni: 1...
  5. Aina ya watu wasiotaka chanjo ya Uviko-19

    Yani nimeangalia kwa makini aina ya watu wanaokwepa chanjo ni kama ifuatavyo. 1. Wengi hawana kazi za kueleweka kwa ujumla ni wabangaizaji 2. Walokole kindakindaki 3. Ambao hawasafiri nje ya nchi hivyo hawajali chochote 4. Wengi wao wana elimu za chini mno
  6. #COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

    Wanabodi, Déclaration of Interest. Mimi Pascal Mayalla ni pro Vaccination ya Covid 19 na nimechanja chanjo ya Corona, na nawahimiza Watanzania, tuchanje. Niko hapa Terminam 3 Airport ya DIA, nimeshuhudia baadhi ya watu wachache wakirudi makwao kwa kakataliwa kusafiri kutokana na kutokuwa na...
  7. C

    #COVID19 Nini kifanyike kuondoa taharuki kwa wanafunzi wanaokimbia ovyo waonapo wageni au magari shuleni?

    Sasa ni taharuki kwa wanafunzi wa shule za msingi wakiwa shule waonapo wageni au magari yakiingia shuleni basi huanza taharuki na kukimbia ovyo. Taharuki hiyo imesababishwa na wazazi wanaowambia watoto wao kuwa serikali inataka kuwachoma chanjo ya Corona kitu ambacho si sahihi. Wazazi hao...
  8. B

    #COVID19 Jumamosi Hospitali ya Amana hawatoi chanjo ya Covid lakini Aga Khan wanachanja, hii ipoje?

    Wiki iliyopita nilijiandikisha online kupata chanjo ya Covid Amana Hosp leo Jmosi Aug 7. Lkn nilipofika pale tuliambiwa leo hawatoi chanjo hadi J'tatu. Baadaye jamaa alinitonya niende Aga Khan. Nikaenda, sikuchukua dak 15 nikapata chanjo. Inakuwaje private hospital wanajali zaidi wananchi...
  9. #COVID19 Ni sahihi Humphrey Polepole kuonesha Msimamo wake wa kutochanjwa?

    Tumeona Viongozi mbalimbali wakitumia hiari yao kuhamasisha watu wakachanjwe na wengine wamekua sehemu ya kuchanjwa kama kuonesha mfano. Polepole Naye yupo na msimamo wake wa kutochanjwa na ameenda mbali akihimiza watu wazingatie vyakula na vilevile kahoji kwanini hii chanjo haioneshi muda...
  10. #COVID19 Geita: Wanafunzi wakimbia ovyo wakiogopa chanjo, Kaimu Mkurugenzi ataka waelimishwe chanjo ni hiari

    Hii ni Tanzania pekee😂😂😂😂 ====== Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Edith Mpinzile, amewaagiza wazazi, walimu na maafisa elimu kutoa elimu kwa wanafunzi kuwa chanjo ya Corona ni hiari na haitolewi kwao kufuatia vitendo vya wanafunzi kukimbia madarasani kila waonapo gari...
  11. #COVID19 Arusha: Watumishi waliofanya igizo kwenye chanjo ya Corona wasimamishwa kazi

    Taarifa kutoka ofisi ya Rais-Tamisemi jioni hii ni kwamba watumishi wawili ambao ni afisa elimu(msingi) na muuguzi msaidizi hospitali ya mkoa wa Arusha wachukuliwa hatua za kinidhamu baada ya video kuvuja wakifanya igizo la chanjo ya corona ambayo watanzania wengi hawaonyeshi kukubaliana nayo...
  12. #COVID19 Arusha: Aliyesimamishwa kwa mzaha wa chanjo ashangazwa na hatua dhidi yake

    Mkuu wa idara elimu msingi halmashauri ya Jiji la Arusha, Omary Kwesiga amesema ameshangazwa kusimamishwa kazi akidaiwa kufanya igizo la kuchomwa chanjo ya ugonjwa wa Covid-19. Amesema picha za video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha kuwa hakuchomwa chanjo hiyo zimechezewa...
  13. Kumbe hata UKIMWI tunaweza kupambana nao kwa chanjo

    Tumemezeshwa kuwa sababu ya kuwa hakuna chanjo ya kirusi cha UKIMWI ni kwa sababu kinabadilikabadilika sana. Lakini tumeona jinsi kirusi cha Korona kinavyobadilika badilika lakini bado wanasayansi wanakaza kuendana nacho, kwa kutengeneza chanjo mpya kila siku. natumaini tutakishinda hiki kirusi...
  14. #COVID19 Chanjo ni kinga dhidi ya maradhi. Kama chanjo ya Uviko-19 sio kinga kwa 100% kwanini tuipigie debe kwa nguvu? Tutakukumbuka hayati JPM

    Tumeambiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kuwa chanjo ya Jonhsonjonhson ni super shot. Maana yake unadungwa shot moja na unakuwa umepata kinga. Wanaoinadi wanatuchanya zaidi kwa kutoa maelezo kuwa hata kama ukipata chanjo hiyo lazima ubaki ukichukua tahadhari kama kuvaa barakoa, kunawa...
  15. K

    Naishukuru Serikali kwa chanjo ya Corona

    Hii ndiyo kazi kweli ya Serikali na nitoe pongezi sana kwa Rais Samia kwa kujali Watanzania kwanza. Wazee wangu na ndugu zangu wamepata chanjo ya covid 19. Nashukuru imetutoa wasiwasi hasa kwa wazazi wetu ambao wapo 70’s. Najua kuna mengi tunalaumu Serikali lakini tunashukuru sasa sana kwa...
  16. J

    Mkuu wa Idara anafanya Igizo la kufifisha juhudi za mwajiri wake katika kuhamasisha chanjo? Huu ni Ugaidi!

    Mkuu wa idara katika halmashauri zetu ni mtu mkubwa sana, yaani boss. Sasa anawezaje kufanya igizo na nesi? Inafikirisha sana yaani kama siyo uhujumu uchumi basi huu ni ugaidi.
  17. A

    Sichanjwi na nikifa roho yangu ikawe laana kwa kila kiongozi aliyesema chanjo ni mbaya

    Habari wadau, leo nimeona niiweke msimamo wangu juu ya chanjo sababu Maneno yamekua Mengi Nasema hivi sichanji chanjo yoyote Ile sababu Serikali yangu ilikuwa kila nikilala nikiamka nakuta kuwa chanjo ya Corona haifai na watanzania tusikubali. Ikiwa kama viongozi wote walishiriki kutuambia hayo...
  18. Yaliyojiri JamiiForums Space kuhusu Maambukizi ya COVID-19 na Utoaji Chanjo Tanzania

    Jamii Forums inakukaribisha kushiriki kwenye Mjadala kuhusu Maambukizi ya #COVID19 pamoja na Utoaji wa Chanjo nchini Tanzania Mjadala huu unafanyika Agosti 6, 2021 kupitia Twitter Spaces (JamiiForums) kuanzia Saa 12 jioni na utahusisha Wataalamu wa Afya watakaozungumzia Masuala anuani kuhusu...
  19. #COVID19 UK: Serikali kutumia kumbi za starehe kuhamasisha vijana kujitokeza kupata chanjo

    Kama jitihada mojawapo ya Serikali kuongeza kasi ya utoaji Chanjo, Vijana wameambiwa wasikubali kupitwa na wakati mzuri ikiwemo uhuru wa kwenda klabu na kusafiri kwa kujitokeza na kupata dozi zote za Chanjo dhidi ya COVID-19. Hatua hiyo inakuja wakati ambapo kuna harakati za klabu kuhamasisha...
  20. B

    #COVID19 Corona: 99% ya vifo Marekani hawakuwa Wamechanjwa

    Mengi yameelezwa kuhusu chanjo za Corona. Kwa mujibu wa balozi wa Marekani, katika vifo vyote vitokanavyo na Corona sasa hivi huko kwao, 99% ni watu ambao hawakuwa wamechanjwa. Angalizo: 1. Ni muhimu ikafahamika kuwa chanjo hizi si dawa ya kutibu au kuzuia mtu kutopata ugonjwa. 2. Chanjo...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…