Michezo ya 19 ya Asia ilifunguliwa tarehe 23 mjini Hangzhou, China. Katika miaka 15 iliyopita, toka Michezo ya Olimpiki ya Beijing, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing hadi Michezo ya Asia ya Hangzhou inayoendelea sasa, China imekuwa mwenyeji wa michezo kadhaa muhimu ya kimataifa...