Kumekuwa na mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuua au kutoua, kufa au kutokufa kwa upinzani Tanzania. Ukiangalia kwa ukaribu jambo hili; kuna watu wanafikiri upinzani ukifa litakuwa jambo la faida kwa taifa, ila kiuhalisia litakuwa ni jambo la hasara kwa watu wote na pengine la hatari...