intaneti

Intaneti (kutoka Kiingereza Internet) ni mfumo wa kushirikiana kwa tarakilishi nyingi unaowezesha watu mbalimbali duniani kuwasiliana baina yao. Kupitia mtandao huo, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe.

Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mitandao ya tarakilishi inayotumia itifaki inayokubalika ya intarnet Suite (TCP/IP). Intaneti hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za wavuti wa ulimwengu mzima (www) na miundombinu ya kusaidia barua pepe.

Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za rununu na runinga, zimeundwa upya kutumia teknolojia za tovuti, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia tovuti (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika tovuti, ubadilishanaji maoni, na kupatikana habari zinapotokea tu. Intaneti imewezesha au kuharakisha uundaji wa aina mpya za mafungamano za kibinadamu kupitia ujumbe mbashara, majukwaa ya tovuti na mitandao ya kijamii.

Kuna mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta wavuti (kama google) au kwa kamusi elezo kama wikipedia.
  1. BARD AI

    Guinea: Serikali yavunjwa, mipaka yafungwa, intaneti yazimwa kwa muda

    GUINEA: Rais wa Mpito, Mamady Doumbouya, amevunja Serikali ya Kijeshi bila kueleza kwa undani sababu za hatua hiyo huku akifanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri kuanzia nafasi ya Waziri Mkuu. Taarifa zinaeleza kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Brigedia Jenerali Amara Camara amewataka Mawaziri wote...
  2. BARD AI

    Senegal: Serikali yazima Intaneti kwa madai ya kuepusha Machafuko na Uchochezi

    SENEGAL: Serikali imetangaza kusitisha Huduma za Intaneti Nchi nzima kwa maelezo kuwa inakusudia kuzuia usambazaji wa taarifa za chuki na uchochezi wa uasi baada ya Rais Macky Sall kuahirisha Uchaguzi Mkuu. Imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa Uchaguzi uliotarajiwa kufanyika Februari 25, 2024...
  3. E

    Bei za vifurushi vya intaneti kuendelea kuwa juu ni ishara ya kubinywa kwa uhuru wa kutoa na kupata taarifa

    Sio mbali sana. Ni miaka mitatu kurudi nyuma bei za vifurushi vya intaneti ilikuwa ya kawaida sana. Kwa 1000 mtu angeweza kupata kifurushi cha GB1 kwa wiki. Leo hii, GB1 ni 3000. Hebu fikiria kwa sasa, ni watu wangapi wameathirika na mabadiliko hayo? Mimi kipindi hicho, kulingana na bei kuwa...
  4. Webabu

    Vita vya intaneti ni vita vyingine Israel ilivyoshindwa mapema huko Gaza. Jifunze mbinu zilizotumika

    Gaza ikiwa ni kama gereza la wazi la muda mrefu imefungiwa na kila kitu kuingia humo chini ya uangalizi wa Israel.Hata mawasiliano pia lazima yapitie Israel. Mara Israel ilipoamua kuingiza askari wa miguu wakiongozwa na vifaru ilijua ingepata hasara kubwa ambazo wasingependa zijulikane na raia...
  5. Webabu

    Houth wa Yemen yapiga Kusini ya Israel. Na wao wakatiwa intaneti

    Hapo jana wanamgambo wa Houth wa Yemen kwa mara nyengine walifanya mashambulizi ya kuvizia kusini mwa Israel kwenye mji wa bandari wa Eliat. Tofauti na mashambulio ya awali ambayo yaliweza kusitishwa angani moja na israel yenyewe na jengine na kibaraka wao Saudia.Shambulio la hapo jana lilifika...
  6. BARD AI

    Waziri Nape: Usajili wa VPN unafanyika ili kuwatambua Watumiaji wa Intaneti

    Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hilo linatokana na ongezeko la Wananchi zaidi ya 50% kutumia Intaneti ambapo kama kuna mtu ana mawazo ya hovyo atatamani kufanya majaribio yake huko, hivyo Serikali imekuwa ikitunga Sheria zitakazowalinda watumiaji wake...
  7. BARD AI

    Nchi 6 zilizotoa Leseni kwa Starlink kutoa huduma za Intaneti yenye Kasi zaidi Afrika

    Zambia imekuwa Nchi ya 6 barani Afrika kuridhia uwekezaji wa Kampuni ya SpaceX kuanza kutoa huduma za Intaneti yenye kasi zaidi kupitia Starlink, hatua inayotajwa kuwa itapunguza urasimu kwa Watoa huduma waliopo pamoja na kuongeza Ubora wa Mawasiliano ya Mtandao. Kampuni ya Starlink...
  8. LIKUD

    Vodacom kifurushi vya intaneti vinaisha haraka sana

    Kifurushi cha 2500 Zamani ilikuwa unakitumia masaa 24 but sasa hivi ukikiweka asubuhi kabla ya saa tisa anatumiwa msg kifurushi kinakaribia kuisha, inafika saa kumi na moja kifurushi kimeisha. Please ni mtandao gani wanatoa vifurushi vinavyo dumu kwa muda elekezi
  9. Miss Zomboko

    Senegal: Huduma ya Intaneti yazimwa baada ya Kiongozi wa Upinzani kuongezewa Mashtaka

    Senegal imezuia upatikanaji wa Huduma za Intaneti kwa kile kilichodaiwa na Waziri wa Mawasiliano kuwa ni kutokana na kuenea kwa "ujumbe wa chuki" kwenye Mitandao ya Kijamii. Hatua hii inakuja baada ya Kiongozi wa Upinzani, Ousmane Sonko kukamatwa Wiki iliyopita na kushtakiwa tena Jumamosi...
  10. BARD AI

    Ripoti: Ushuru kwenye 'Bando' za Intaneti' ni balaa Tanzania

    Ripoti ya robo mwaka unaoishia Machi 2023 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha gharama za ushuru wa bando la intaneti zimeongezeka ikiliganishwa na kipindi kama hiko Machi 2022. Machi 2022 kwa kila MB moja ushuru uliokuwa unakatwa ni shilingi mbili ambayo imeongezeka hadi...
  11. BARD AI

    Mapigano yasababisha huduma za Intaneti kuzimwa Sudan

    Mtandao wa #NetBlocks umeripoti kuwa Vita ya pande mbili za Majeshi zinazopigana Nchini #Sudan imesababisha upatikanaji wa huduma ya Mawasiliano ya Intaneti kushuka hadi kufikia 2%. Mapigano hayo yaliyoanza Aprili 15 kati ya vikosi vinavyomtii Mkuu wa Jeshi, Abdel Fattah al-Burhan na vya Makamu...
  12. J

    Matumizi ya Intaneti: Changamoto za gharama na ubora wa huduma zisifumbiwe macho

    Ili Jamii inufaike kikamilifu na Intaneti, changamoto kama Ubora wa Huduma na Gharama hazipaswi kufumbiwa macho Maisha ya Wananchi wengi yamebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na Upatikanaji wa Intaneti. Uwepo wake unawezesha kufurahia Haki nyingine za Msingi za Binadamu
  13. The Sheriff

    Dhamira ya Kuhakikisha Kila Mmoja Ananufaika na Huduma ya Intaneti Bado Inakwamishwa Sehemu Mbalimbali Duniani

    Serikali kwa kushirikiana na watoa huduma wanaweza kuzuia huduma ya kufikia mtandao kwa njia nyingi. Kwa mfano, serikali zinaweza kukata gridi ya umeme au kuhujumu miundombinu ya huduma ya mtandao kama vile minara ya simu za mkononi na kebo za fibre optic. Serikali pia zinaweza kuzuia ufikiaji...
  14. Cannabis

    Waziri Nape: Hatujaibania starlink kutoa huduma ya intaneti, Elon Musk bado hajakidhi vigezo tulivyomuwekea

    Waziri Nape Nnauye amesema hawajaibania Starlink kutoa huduma ya intaneti nchini bali ni kuwa Kampuni hiyo inayomilikiwa ns tajiri Elon Musk haijakidhi vigezo ilivyowekewa na serikali ikiwamo kufungua ofisi nchini Tanzania. Amesema vigezo hivyo vimewekwa na serikali ili kumlinda Watanzania...
  15. beth

    Gharama kubwa za Vifurushi vya Intaneti ni kikwazo kwa Waafrika

    Kwa mujibu wa Ripoti ya Statista, Waafrika wengi wanashindwa kutumia Intaneti kutokana na gharama ya Huduma hiyo kuwa kubwa Wananchi kutoka Mataifa mbalimbali Barani humo wanategemea Mtandao ili kupata Huduma muhimu, lakini wanatumia gharama kubwa ili kuweza kupata Intaneti Gharama zinapokuwa...
  16. J

    Bila umeme wa uhakika, tunawezaje kunufaika na Teknolojia?

    Umeme ni hitaji la Msingi katika kufikia na kutumia Teknolojia, ikiwemo Intaneti Kama Mwananchi unayetumia au kutegemea Digitali kwa shughuli mbalimbali, unaathirika kwa kiwango gani unapokosa Umeme?
  17. J

    Intaneti ina nafasi muhimu katika kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kufurahia Haki ya Kupata Taarifa

    Asilimia kubwa ya Watu wenye Ulemavu bado wapo nje ya Mitandao kwasababu wanashindwa kumudu gharama na kukosa Miundombinu ya kuwasaidia kutumia Vifaa vya Kidigitali. Hatua zinatakiwa kuchukuliwa kuhakikisha wanaweza kumudu na kufikiwa na Intaneti. Pia ni muhimu kuimarisha Matumizi ya Teknolojia...
  18. beth

    Athari zitokanazo na kuzima Mtandao zisipuuzwe. Biashara Nchini Ethiopia zapoteza Dola za Marekani Milioni 145.8

    Ripoti Mpya iliyochapishwa na Shirika la Top10VPN inasema kukosekana Mtandao huko Tigray, Ethiopia Mwaka 2022 kumezigharimu Biashara Nchini humo Dola za Marekani Milioni 145.8 Kuzuia Intaneti pamoja na kuweka vikwazo katika Upatikanaji wake huwaathiri Wananchi Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa...
  19. LA7

    Mko wangapi kwenu mnaotumia mitandao ya kijamii?

    Sio kwamba najisifia la! hasha! Kuna wakati huwa natamani hata kaka yangu au dada yangu au ndugu wengine wa karibu waone au wasome nilichokiweka mtandaoni lakini inakuwa ngumu. Katika familia yangu baba ana wanawake wa nne hivo watoto jumla tulio hai tupo 27, mimi ni wa 5 upande wa mama yangu...
  20. J

    60% ya Raia Barani Afrika hawapo Mtandaoni

    Afrika ni eneo liliounganishwa na Intaneti kwa kiwango kidogo zaidi, ikielezwa takriban 60% ya Raia hawapo Mtandaoni. Hii inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo gharama, Ujuzi kuhusu matumizi yake pamoja na uhaba wa Miundombinu unaokwamisha ufikiaji wa Huduma hiyo. Barani Afrika na Duniani...
Back
Top Bottom