intaneti

Intaneti (kutoka Kiingereza Internet) ni mfumo wa kushirikiana kwa tarakilishi nyingi unaowezesha watu mbalimbali duniani kuwasiliana baina yao. Kupitia mtandao huo, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe.

Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mitandao ya tarakilishi inayotumia itifaki inayokubalika ya intarnet Suite (TCP/IP). Intaneti hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za wavuti wa ulimwengu mzima (www) na miundombinu ya kusaidia barua pepe.

Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za rununu na runinga, zimeundwa upya kutumia teknolojia za tovuti, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia tovuti (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika tovuti, ubadilishanaji maoni, na kupatikana habari zinapotokea tu. Intaneti imewezesha au kuharakisha uundaji wa aina mpya za mafungamano za kibinadamu kupitia ujumbe mbashara, majukwaa ya tovuti na mitandao ya kijamii.

Kuna mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta wavuti (kama google) au kwa kamusi elezo kama wikipedia.
  1. beth

    Nape: Kampuni za simu haziibi vifurushi vya intaneti vya wateja

    Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Bungeni kuwa Serikali inaendelea kuchambua malalamiko ya matumizi ya Bundle kwenye simu. Amefafanua, "Malalamiko kwamba kuna Bundle zinawekwa kwenye Simu, zinatumika bila Mtumiaji kuzitumia yamekuwepo, yamefikishwa...
  2. beth

    Teknolojia na Afya ya Akili: Kwanini matumizi yaliyopitiliza huweza kuwa na athari mbaya

    Kwasababu ya muda ambao watu hutumia mtandaoni, ni muhimu kuelewa uhusiano kati ya Afya ya Akili na Teknolojia, kwani mbalimbali Tafiti zinaonesha matumizi ya Intaneti kupita kiasi yana madhara. Mitandao ya Kijamii ni mojawapo ya njia kuu ambazo Intaneti huathiri Afya ya Akili. Hii hutokea...
  3. Jonh-B

    Natamani kujifunza mengi zaidi kuhusu namna ya kuingiza hela kwa kutumia intaneti

    Habari nduguzanguni, Kwa hekima nawaombeni mnisaidie kuhusu hili jambo kuwa mitandao na internet kuna fursa za kujipatia pesa na ukaishi kwa kupunguza stress za maisha kwa access ya internet! Tangu nimesikia kuhusu hili na kukomaa kufatilia youtube chanel tofautitofauti na sehemu nyingine na...
  4. beth

    Burkina Faso yasitisha huduma za intaneti kutokana na maandamano

    Serikali Nchini Burkina Faso imeongeza muda wa kusitishwa Huduma za Intaneti, ikielezwa hatua hiyo inatokana na sababu za Usalama na Ulinzi wa Taifa. Huduma za Intaneti zilikatwa kutokana na maandamano dhidi ya Serikali na Vikosi Washirika vya Ufaransa baada ya Maafisa 49 wa Jeshi la Polisi na...
  5. instagram

    Serikali zenye bando za gharama kubwa zinazalisha vijana maskini kwa kuwanyima intaneti isiyo na kikomo

    INFORMATION IS POWER Miaka yote mkoloni ametumia udhaifu wa information kuwatawala waafrika na viongozi wa kiafrika bila kujua wameingia kwenye mtego wa mabeberu kwa kuwaminya wananchi wao taarifa. Tangu Uhuru africa tumebaki nyuma kwa kukosa vitabu vyenye ubora kulinganisha na wenzetu wazungu...
  6. mshale21

    Gerson Msigwa: Iko nchi Ulaya GB1 unanunua kwa Dola 15

    "Kumekuwa na malalamiko ya vifurushi vimepanda, lakini niwaambie sisi ni kati ya nchi 5 Afrika zenye gharama za chini za bando, ziko baadhi ya nchi za Ulaya ambazo gharama zake ni kubwa, ninafahamu iko nchi ambayo unanunua GB 1 kwa Dola 15" ------- Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa...
  7. Chief-Mkwawa

    Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

    Kutokana na Uhaba wa Vifurushi kwa sasq, vifurushi vizuri vinapatikana Tigo postpaid na Airtel Sme. Airtel SME. Tigo postpaid Namna ya kupata official hivi vifurshi, tembelea wakala wa mtandao husika wa karibu ukiwa na Tin no, leseni na kitambulisho. Kama huna details hapo juu wapo...
Back
Top Bottom